Wednesday, 25 February 2015

UGONJWA WA KISUKARI, SABABU NA DALILI ZAKE
Kisukari ni ugonjwa unaotokana na matatizo ya mfumo wa umeng’enyaji wa chakula, Sukari nyingi mwilini au katika damu. Kwa kawaida mwili una kiwango mahususi cha mahitaji ya glukozi.Leo hii tutakufahamisha baadhi ya sababu zinazoweza kukusababisha ukapata ugonjwa wa kisukari.

Visababishi hivyo ni pamoja na matumizi ya sukari nyingi, kurithi kutoka kwa wazazi na vyakula vya mafuta,  kutokupenda kufanya mazoezi  na unywaji wa pombe kupita kiasi.

Sababu nyingine ni anasa, starehe na mtindo wa maisha ya kubweteka sambamba na kula vyakula vilivyotengenezwa kwa kuongezwa sukari, hususani vyakula vya viwandani.

Dalili ambazo huweza kuonekana kwa mtu mwenye ugonjwa wa kisukari ni pamoja na kuhisi kiu, kukauka mdomo, ulimi na kujikuta unakuwa na hamu ya kunywa maji mara kwa mara.

Kwenda haja ndogo (kukojoa) mara kwa mara hasa usiku pamoja na kujihisi mchovu licha ya kutofanya kazi yoyote.

Pia wengine huanza kupoteza uwezo wa kuona vizuri, kushindwa kushiriki tendo la ndoa, baadhi ya viungo kufa ganzi kama vile mikono na kuhisi inawaka moto, kuumwa na kichwa na kutokwa na jasho mara kwa mara na hasa usiku.

Hali kadhalika, mhusika anaweza kuwa mwenye hasira za mara kwa mara pamoja na kuwa msaulifu mara kwa mara.

 Sasa tupo tayari kuanza kupokea matangazo ya biashara yako yoyote na kukuwekea kwenye tovuti hii inayotembelewa na maelfu ya watu. Karibu sana gharama zetu ni nafuu sana piga simu namba 0758 163 818, 0672 060 006, Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment