Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 11 February 2015

UHABA: JE, UNAFAHAMU DAKTARI MMOJA ANAHUDUMIA WAGONJWA WANGAPI HAPA NCHINI?
IMEELEZWA kuwa tatizo la uhaba wa madaktari nchini bado ni changamoto kubwa linalohitaji ufumbuzi wa kina zaidi kwa kuongeza jitihada za kuzalisha madaktari wengi watakaofanya kazi nchini.
Hayo yamesemwa na Rais Jakaya Kikwete mjini Moshi akizindua jengo la upasuaji katika Hospitali ya Mawenzi pamoja na kuweka jiwe la msingi jengo la wodi ya kinamama na watoto, ambapo alisema  tatizo hilo ni kubwa na serikali yake imejipanga na kuweka mikakati ya kulitatua.

Alisema kuwa, kwa sasa daktari mmoja anahudumia wagonjwa 30,000 na muuguzi anahudumia wagonjwa 23,000 wakati hali ikiwa hivyo hapa nchini, wenzetu katika nchi za Ulaya, daktari mmoja anahudumia wagonjwa 5,000.

Katika kukabiliana na tatizo hilo Rais Kikwete alisema, njia pekee ya kukabiliana na changamoto hiyo ni kuzalisha madaktari wengi watakaofanya kazi nchi nzima.

Mbali na hayo, aliendelea kusema kuwa, kwa sasa serikali imekuwa ikijenga uwezo wa ndani wa kukabiliana na magonjwa ikiwamo malaria, lakini licha ya jitihada hizo za serikali za kupambana na ugonjwa huo bado kumekuwa na baadhi ya wananchi wakitumia vyandarua wanavyopewa kujikinga na mbu wao wanafugia kuku pamoja na kuweka kwenye bustani za mbogamboga.

Ikiwa ni wewe au ndugu , rafiki, jirani yako anasumbuliwa na magonjwa sugu unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata matibabu kwa kutumia dawa zetu za asili zisizo na aina yoyote ya kemikali na ni salama kwa matumizi ya binadamu.

No comments:

Post a Comment