Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 25 February 2015

UMEISIKI HII YA MWALIMU AMBAYE AMEKUWA AKIKAA NA KINYESI PASIPO KUJALI HATIMA YA AFYA YAKEHalmashauri ya Manispaa ya Temeke imeamua kuingilia kati tukio la Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila, Gaudensia Albart kukaa na kinyesi, mende, funza ndani ya muda wa miaka miwili na kutaka kumchukulia hatua zaidi.


Tukio hilo la mwalimu huyo kuishi na mrundikano wa uchafu huo liligundulika siku tatu zilizopita eneo la Yombo Kisiwani, Kata ya Sandari wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari hapo jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Afya wa kata hiyo, Vaico Maloni alisema siku ya jana ndio walipanga kuteketeza uchafu huo, lakini walishindwa kufanya hivyo kutokana na  kukosa vifaa vya kutosha vya kufanyia zoezi hilo.

Maloni alisema kuwa wameamua kuomba msaada wa wataalam kutokana na tatizo hilo ni kubwa na lenye kuhitaji vifaa vya kisasa ili kuweza kuchukua tahadhari zaidi.

Jinsi tukio hili lilivyotokea
Mmiliki wa nyumba aliyopanga mwalimu huyo, Ruben Shayo alliliambia gazeti moja hapa nchini kuwa Februari 22 mwaka huu,  ulionekana moshi kwenye chumba cha mwalimu huyo, ambapo wapangaji wengine walimjulisha na kwenda kuushuhudia moshi huo ili kuweza kujua chanzo chake.

Alisema baada ya kufika kwenye chumba hicho waliona moshi mwingi ukitokea  madirishani na kufanya juhudi za kuingia ndani ili kuuzima moto huo huo, ambapo walijaribu kumuita mwalimu huyo kwa muda mrefu pasipo majibu, lakini mwalimu huyo hakutoka hadi pale walipomwambia kuwa watakwenda polisi.

Baada ya kuitikia, ilibidi kumuita mwenyekiti wa mtaa ili waweze kuingia ndani kwake kuangalia hali ivyo kwenye chumba chake, "tulipoingia ndani tukakutana na nguo zikiwa zimezagaa na kuonekana kuwa alikuwa akichoma nguo zake” alisema.

Mbali na hayo pia waliona vyombo mbalimbalia ambavyo vilikuwa  vimehifadhiwa kinyesi na mkojo, huku kukiwa na funza na mende wakiwa wamezagaa hadi kitandani.
Pamoja na hayo alivitaja baadhi ya vyombo ambavyo alikuwa amehifadhia kinyesi hicho ni ndoo, sufuria, chupa na mabeseni  na harufu kali ya kinyesi ikitapakaa  ndani.  
Tukio hilo limeonekana la kustahajabisha kwa waliowengi kutokana na kitendo cha mwalimu huyo kuishi na uchafu huo ndani ya nyumba yake.

Sasa tupo tayari kuanza kupokea matangazo ya biashara yako yoyote na kukuwekea kwenye tovuti hii inayotembelewa na maelfu ya watu. Karibu sana gharama zetu ni nafuu sana piga simu namba 0758 163 818, 0672 060 006, Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com 

No comments:

Post a Comment