Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 25 February 2015

UMUHIMU WA KUFANYA MAZOEZI KWA MAMA MJAMZITO

Mazoezi ni muhimu katika maisha ya kila siku ya binadam, lakini mazoezi kwa mama mjamzito humuandaa mama na kumpa nguvu wakati wa kujifungua.


Mama mjamzito anapofanya mazoezi, humsaidia kutanua misuli ya kiuno na ile ya njia ya uzazi. Hivyo mazoezi  huipa nguvu na uvumilivu  misuli wakati wa kujifungua.
Aidha, misuli inapokuwa mwepesi, huwa ni rahisi mwili huo kurudi katika umbile lake la awali mapema mara baada ya kujifungua.

Aidha, mjamzito anapofanya mazoezi, huufanya moyo wake kupata mapigo mazuri na kuchochea mzunguko mzuri wa damu, huku mazoezi pia yakimsaidia mam mjamzito asiongezeke uzito na kumuepusha na shinikizo la damu.

Kuna mazoezi ambayo ni mazuri kwa mama anayetarajia kupata mtoto, licha ya kuwa baadhi ya mazoezi huenda yasiwe na matokeo mazuri kwa mama ambaye amebakiza siku chache za kujifungua. Hivyo, mama hutakiwa kuhakikisha anawasiliana na daktari wake kabla hajafanya uamuzi wa aina ya mazoezi ya kufanya.

Miongoni mwa mazoezi ambayo huweza kumsadia mama ni pamoja na kutembea, ambako humsaidia mjamzito asitetemeke magoti na kifundo cha mguu.

Zoezi hili la kutembea linaweza kufanyika popote na halihitaji zana, wala fedha. Isipokuwa viatu visivyo na kisigino, huku kutembea huko kutembea huko kukiweza kufanyika hata katika hatua za mwisho za ujauzito.

Kuogelea pia ni zoezi jingine ambalo linaweza kufanywa na mama mjamzito, ambapo wataalam wanasema kuwa kwa kufanya zoezi hili husaidia kuipa nguvu misuli mikubwa ya mwili hasa ya mikono na miguu.

Pia, kuogelea huepusha maradhi ya moyo na humfanya mjamzito kujihisi mwepesi licha ya kilo za ziada alizonazo.

Mama mjamzito akifanya mazoezi ya kuogelea

Lakini katika zoezi hili inashauriwa mama mjamzito kuwa na muangalizi ambaye anaujuzi  mzuri wa kuogelea ili mama aweze kuwa salama zaidi katika zoezi hilo.

Kesho Februari 26, 2015 nitakufahamisha mambo matano ya kuzingatia kabla ya kufanya mazoezi tafadhali endelea kuwa karibu na tovuti hii kila siku.
 

No comments:

Post a Comment