Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 16 February 2015

UNAPOPATWA NA UGONJWA WA TETEKUWANGA TUMIA ASALI KAMA TIBA
Tetekuwanga huu ni ugonjwa ambao hautofautiani sana na surua kutokana na ugonjwa huu nao kuwashambulia sana watoto wenye umri wa chini ya miaka saba.


Ugonjwa huu unaambukiza kwa haraka sana, hususani pale ambapo unaonekana kwamba unaelekea kupona.

Dalili za tetekuwanga ni pamoja na hali ya kuhisi  kuwa na homa, kuumwa kichwa, kusikia uchovu wa mwili, kuonekana kwa vipele kifuani aua sehemu ya juu ya mgongo na hatimaye upele unaofanana na malengelenge husambaa mwili mzima.

Hata hivyo, baada ya siku chache upele huo hutumbuka na kuanza kukauka na hapo mgonjwa  huweza kuanza kupona kwa kipindi cha siku kumi hadi ishirini.

Ugonjwa huu wa tetekuwanga ni ugonjwa unaoenea kwa njia ya virusi, hata hivyo mtaalam wa tiba asilia kutoka Mandai Herblist Clinic Dk Abdallah Mandai, anasema ugonjwa huo huweza kutibika kwa kutumia asali na giligiliani.

Kuhusu tiba hizo, Dk Mandai anafafanua kuwa, ili kusaidia kuharakisha kupona kwa vidonda vya upele, kwa muda wa siku tatu mgonjwa anatakiwa apake asali mwili wote.

Tiba nyingine ni ile ya giligiliani ambapo inapaswa kupondwa pamoja na karoti na kuchanganywa na maji kisha chemsha kwa dakika 10 na uchuje na kunywa maji yote kwa siku moja. Endeleza tiba hiyo kwa siku nne.

Unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic endapo unasumbuliwa na magonjwa yoyote na hakika utapata tiba nzuri na sahihi na kupona kabisa shida inayokusumbua. Kliniki ipo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.Au piga simu namba, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment