Friday, 20 February 2015

UNAUJUA MNANAA? NI MMEA WENYE SIFA YA KUTIBU MAGONJWA MENGI
Mnanaa ni mmea ambao unapatikana sana katika nchi mbalimbali ikiwemo za hapa Afrika Mashariki, huku wengi wakiutumia mmea huu kwa kuupanda kama maua katika nyumba zao pamoja na bustanini.


Mmea huu huwasidia sana kinamama ikiwemo kuondoa maumivu wakati wa hedhi, kizazi kuuma pamoja na kuongeza maziwa kwa kina mama wanaonyonyesha.

Aidha, mnanaa pia husaidia watu wenye tatizo la misuri inayokaza ama kustuka , kutuliza maumivu ya sikio, kutuliza maumivu, sambamba na kutibu homa ya manjano.

Mnanaa pia husaidia maradhi ya koo, minyoo kwa watoto wenye chai yake,kuzui kichefuchefu na kutapika, kutoa gesi tumboni na kuzuia kuharisha na matatizo ya tumbo.

Hata hivyo, mnanaa bado unauwezo wa kutibu maradhi mengi zaidi ambayo ni pamoja na matatizo ya meno, ambapo mhusika hupaswa kusukutua au kutafuna mmea huo, huku ukifahamika kwa kuwa dawa nzuri ya kulinda meno yasiweze kumeguka  au kung’oka  na kuvuja damu kwenye fizi.


Mbali na hayo, mnanaa hushusha joto la mwili na kutibu ugonjwa wa tambaza na minyoo kwa watoto ambao hupaswa kunywa chai yake, huku ukielezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia mtoto kukojoa kitandani.

Endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu basi wasiliana na Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 

1 comment:

  1. majani haya ndiyo yanayo itwa korianda? au nimche mwingine?

    ReplyDelete