Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 5 February 2015

USHUHUDA,POMBE ILINIFANYA NIPOTEZE KAZI SERIKALINI BAADAYE TIBA KUTOKA KWA DK MANDAI IKANIOKOA
Pombe ni moja ya kinywaji chenye kileo na kinachopendwa na watu wengi, licha ya kuwa na madhara makubwa katika afya ya mwanadamu.

Mbaya zaidi unapoanza kutumia pombe huwa ni jambo rahisi sana, lakini shida inakuja pale unpohitaji kuacha kutumia kinywaji hicho.

Leo nakukutanisha na Bw, Sospeter Makingi aliyewahi kuwa mlevi wa kupindukia, lakini kwa sasa hagusi pombe na anaichukia hata harufu yake baada ya kutumia dawa kutoka Mandai Herbalist Clinic.

Kitengo cha habari cha kliniki hii kimefanya mahojiano na Bw, Sospeter Makingi, na mahojiano hayo yalikuwa kama ifuatavyo……..Karibu.
 
Kitengo cha habari: Bwana Sospeter Makingi karibu katika kitengo chetu cha habari hapa Mandai Herbalist Clinic.

Makingi: Asante sana.

Kitengo cha habari: Nimepata habari kwamba ulikuwa ni mnywaji wa pombe sana na sasa umeacha hebu tuambie nini kilitoke hadi ukaacha? 

Makingi: Mimi kwa mara ya kwanza nilikuja hapa (Mandai Herbalist Clinic) ilikuwa mwaka 2012 na lengo langu lilikuwa ni kupata dawa ya kunisaidia kuacha pombe na kwa kipindi hicho nilikuwa nishahangaika na dawa mbalimbali bila kufanikiwa, lakini nilipofika hapa nikaonana na Dk Mandai kwa mara ya kwanza.

-Nakumbuka daktari jambo la kwanza aliniuliza “Je unataka uache kunywa pombe haraka haraka au pole pole” nilimjibu kuwa nataka kuacha pole pole na nikiacha niwe nimeacha kabisa kwa sababu hiyo ya kuacha haraka nilihisi naweza baadaye tena kuwa na kiu.

-Basi baada ya kuongea hayo dokta alinipa dawa na maelekezo ya jinsi ya kuitumia na ilikuwa ni dawa ya kuchanganya kwenye uji au chai, lakini nilipotumia dawa ndani ya wiki ya kwanza nikajikuta ile kiu ya pombe ikaanza kupotea taratibu na ilipokatika wiki ya pili nilikuwa sitamani kabisa kunywa pombe hata harufu yake pia.

-Kwa sasa nina kama mwaka mmoja na miezi sita sijanywa pombe wala kukanyaga bar.

Kitengo cha habari: Ni sababu gani zilikuhamasisha kuacha pombe?

Makingi: Kikubwa zaidi pombe iliniharibia kazi zangu nyingi, hivi tunavyozungumza hapa, mimi nilikuwa ni muajiriwa wa serikalini maana nilikuwa nafanya kazi pale hazina Wizara ya Fedha kabisa na nilikuwa kama askari pale. Lakini pombe iliharibu kazi yangu hicho kitu kiliniuma sana, ukizingatia nilikuwa nimepangiwa na serikali kustaafu mwaka 2025 yaani miaka 10 mbele kutoka leo hii.
Bwa Sospeter Makingi kushoto akizungumza na Kenneth Maganga ambaye ni Msimamizi wa Kitengo cha Habari kutoka Mandai Herbalist Clinic
Mahojiano kati ya Bwa Sospeter Makingi na Kenneth Maganga yakiendelea kuhusu namna bwana huyo alivyoweza kuacha pombe kabisa kupitia dawa za Mandai Herbalist Clinic
Makingi anaendelea kueleza- Nilipofukuzwa kazi nikajikuta nimezidi zaidi kunywa pombe kutokana na hasira na hivyo nikajikuta nimeharibu maisha yangu kabisa na kuyumba kiuchumi zaidi.


-Hata hivyo, ni kama Mungu alikuwa na mimi maana nilikuwa na bahati ya kupata kazi nzuri katika makampuni binafsi kutokana na vyeti vyangu, lakini bado kwenye kampuni hizo nilikuwa sidumu zaidi ya mwaka pombe inaharibu.

-Kwa mfano mwaka 2001 nilipata kazi kwenye kampuni moja ya ulinzi, lakini pombe ikaharibu kazi hiyo. Pia nikapata kazi nyingine kwenye kampuni ya kupaki magari iitwayo ‘Tanzania Parking System’ tena wakati inaanza tu na sisi ndio tulikuwa askari wa kwanza kwa ajili ya kuhimiza watu wapaki magari katika maeneo ya kulipia, lakini bado pombe pia iliharibu hiyo kazi.

Kitengo cha habari: Sasa baada ya yote hayo ikawaje?

Makingi: Sasa tangu hapo nikawa ni mtu wa kuingia kwenye vikampuni vidogo vya kijinga jinga ilimradi tu siku iende.

-Hapo ndipo mimi mwenyewe nikaona kuwa bila kuacha pombe siwezi kufika popote, maana hata mke wangu na ndugu zangu walikuwa wananishangaa wakawa wanahisi labda nimerogwa. Kwa hiyo kwa ujumla hayo ndio yalinifanya nisake tiba kwa udi na uvumba nakujikuta nimefika hapa Mandai Herbalist Clinic na kupata dawa na kuachana na pombe kabisa.

Kitengo cha habari: Ushauri wako kwa wale wanokunywa pombe, lakini wanatamani kuacha?

Makingi; Kuacha pombe ni maamuzi ya mtu binafsi kwa sababu kama mimi nisingekuja hapa kwa Dk Mandai basi nisingepona kwa maana Dk Mandai asingenifuata nyumbani kwangu.

-Kwa mfano mimi saizi hata familia yangu ina amani na hata mke wangu kanenepa saizi, kwahiyo haijarishi unakipato kiasi gani pombe ni kero tuu!

-Pombe ni tamu wakati ukiwa bar unakunywa unaongea na wenzako na hela unazo kidogo, lakini kwa familia zetu ni kero kubwa, pombe inarudisha maendelea nyuma mfano mimi hadi sasa umri huu bado naishi nyumba ya kupanga!

Kitengo cha habari:Pole sana Bw, Makingi lakini tunaamini sasa utafanya mambo mazuri ya maendeleo kwani pombe umeacha kabisa sisi tukutakie kila lililojema.

Endapo na wewe unatatizo kama la Bw Sospeter Makingi unaweza kufika Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam kwenye kliniki ya Mandai Herbalist Clinic ili ujipatie tiba yako ya kuacha pombe sasa maana madhara yake ni mengi kwa afya.


No comments:

Post a Comment