Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 26 February 2015

UTAFITI: DAWA ILIYOELEZAWA KUWA NA UWEZO WA KUZUIA VIRUSI VYA HIV KWA WANAWAKE IMEELEZWA KUWA HAIFAI
Dawa iliyowahi kukisiwa kuwa na uwezo wa kupunguza uwezekano wa mwanamke kupata virusi vya UKIMWI wakati wa kushiriki tendo la ngono imeelezwa kuwa haifai.


Hayo yameelezwa baada ya kufanyika kwa utafiti mkubwa uliofanywa na Shirika la Follow on Africa Consortium for Tenofovir kutoka Afrika kusini.

Matokeo ya utafiti huo unaojulikana kama facts 001 yalitolewa katika kongamano la magonjwa ya virusi na yale ya maambukizi nchini Marekani.

Kwa mujibu wa gazeti la Mail and Guardian nchini Afrika kusini, wanawake katika utafiti huo waliagizwa kujipaka dawa hiyo katika sehemu zao za siri kabla na kila baada ya tendo la ngono.

Hata hivyo, matokeo hayo yanapinga matokeo ya utafiti mwingine uliochapishwa mwaka 2010 na Shirika la Mpango wa Utafiti wa Ugonjwa wa Ukimwi nchini Afrika kusini Caprisa.

Inaelezwa kuwa watafiti waliwatumia zaidi ya wanawake 900 katika jimbo la Kwa Zulu Natal na kuripoti dawa hiyo ya Tenofivir ilikuwa na uwezo wa asilimia 39 pekee wa kupunguza viwango vya maambukizi ya viini vya HIV miongoni mwa wanawake hao.

Viwango vya maambukizi ya HIV nchini Afrika kusini vilikuwa kwa asilimia 12.2 mwaka 2012 ikiwa ni kiwango cha juu zaidi duniani kulingana na utafiti wa Baraza la Sayansi ya Binaadamu kuhusu kinga ya HIV, visa na tabia.

Kutokana na viwango hivyo kuwa ni vya juu miongoni mwa wanawake na kusababisha utafiti kutafuta tiba za kinga zinazowalenga wanawake kama vile dawa inayopakwa katika sehemu za siri, pamoja na sindano zilizojaa tiba za kukabiliana na HIV.

Aidha, taarifa zinaarifu kuwa, wakati wa utafiti huo uliochukuwa takriban miaka mitatu,watafiti waliwatumia wanawake 2000 wasio na virusi vya Ukimwi wemye umri kati ya miaka 18 hadi 30, na kuwapatia nusu yao dawa ya Placebo na nusu nyengine wakapewa dawa ya kwenye sehemu za siri ‘tenofivir’, ambayo ni dawa ya kukabiliana na virusi vya Ukimwi.

Baadaye watafiti hao walipima viwango vya maambukizi ya virusi vya HIV kati ya makundi hayo mawili na kubaini kwamba wanawake waliopewa dawa hiyo ya ‘tenofivir’ waliambukizwa virusi vya Ukimwi sambamba na wanawake waliopewa dawa kupaka ya placebo.

Kwa jumla wanawake 123 waliambukizwa virusi vya HIV huku 61 wakiwa ni wale waliopewa mafuta ya ‘tenofivir’ na 62 wakiwa walipewa mafuta ya ‘placebo’

Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment