Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 27 February 2015

UTAFITI: WANASAYANSI WANAMPANGO WA KUANZA UPANDIKIZAJI WA VICHWA VYA BINAADAMU IFIKAPO 2017Wanasayansi wamesema wanaamini kuwa upasuaji wa upandikishaji wa kichwa cha mwanadamu katika mwili mwingine huenda ukafanikiwa.

Mradi huo unatarajiwa kuzinduliwa na madaktari katika kongamano wakati wa msimu wa joto, kwa lengo la kuanzisha utaratibu huo mnamo mwaka 2017.

Taarifa zinasema kuwa mpango huo utaongozwa na daktari raia wa Italy Sergio Canavero ambaye anatoka katika kundi moja la wanasayansi mjini Turin.

Daktari huyo anaamini kwamba upandikishaji wa vichwa vya watu utawasaidia wale wanaosumbuliwa na magonjwa ya misuli na saratani.

Baada ya kutoa wazo hilo mnamo mwaka 2013,daktari Canavero anaamini vikwazo vikuu vya upasuaji huo vimekabiliwa, kulingana na ripoti mpya ya wanasayansi.

Vikwazo hivyo ni pamoja na usimamizi wa uti wa mgongo kuingiliana na kichwa kipya pamoja na kuhakikisha kuwa kinga ya mwili haikikatai kiungo hicho kipya.

Daktari Canevaro alichapisha taarifa iliokuwa na nadharia kuhusu vile anavyoamini upasuaji huo unaweza kufanyika.
   

Sasa tupo tayari kuanza kupokea matangazo ya biashara yako yoyote na kukuwekea kwenye tovuti hii inayotembelewa na maelfu ya watu. Karibu sana gharama zetu ni nafuu sana piga simu namba 0758 163 818, 0672 060 006, Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com

 

No comments:

Post a Comment