Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 20 February 2015

WANASAYANSI:CHANJO DHIDI YA HIV YAONESHA MAFANIKIO

Wanasayansi wa nchini Marekani wamesema kuwa chanjo mpya dhidi ya virusi vya  HIV imeonekana kuwa na uwezo wa kuwakinga nyani dhidi ya virusi vya ugonjwa huo.


Taarifa zinaarifu kuwa, majaribio yaliofanywa miongoni mwa nyani hao katika ripoti ya jarida la asili, yalionesha kuwa nyani walikingwa kutokana na aina yoyote ya virusi vya HIV kwa kipindi cha wiki 34.

Kufuatia hali hiyo kikosi hicho cha wanasayansi hao kimeitaja hatua hiyo kama moja ya  mafanikio makubwa na sasa wapo katika mpango wa kuanzisha mbinu hiyo miongoni mwa binaadamu.

Pia watafiti wamesema wanaamini kuwa mpango huo huenda ukawa muhimu miongoni mwa watu ambao wana virusi vya HIV.

Naye mtafiti bingwa Professa Micheal Farza aliiambia BBC kuwa, “tunakaribia kupata tiba, lakini bado tunakabiliwa na vikwazo hususani katika salama wa kuwapa watu wengi zaidi.”

Hata hivyo, inaelezwa kuwa chanjo za HIV zimekuwa zikishindwa kufanikiwa kutokana na virusi hivyo hujibadilisha mara kwa mara kila vinapolengwa na dawa. Lakini chanjo hii mpya hulenga eneo ambalo virusi hivyo hujibadilisha.

Mbali na hayo, watafiti katika Taasisi ya Scripps mjini California wamebadilisha DNA ya nyani hao ili kuzipa seli zao uwezo wa kukabiliana na virusi vya HIV.

BBC

No comments:

Post a Comment