Monday, 2 February 2015

ZIFAHAMU FAIDA ZA LIMAO KAMA TIBA
Limao ni tunda dogo ambalo mara nyingi hutumika jikoni katika shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukata shombo katika vyakula mbalimbali mfano samaki. Asili ya tunda hili ni Asia.

Mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai anasema kuwa, zipo faida nyingi  za kutumia limao, hasa wakati wa asubuhi wakati mwili umekaa bila kula usiku kucha, miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kuusaidia mwili katika suala la mmeng’enyo wa chakula na kulifanya ini liweze kufanya kazi vizuri.

Mtaalam huyo anaeleza kuwa limao pia huwasaidia wale wenye matatizo ya tumbo, malaria, dosari katika figo, kiungulia na kuongeza hamu ya chakula.

Aidha, Dk Mandai anasema kuwa limao husaidia wale wenye matatizo ya tumbo, kikohozi, mafindo findo, mafua, kisukari,  homa pamoja na kusaidia kuleta harufu nzuri kinywani hii ni kwa sababu aside iliyopo kwenye maji ya limao husaidia kuua bacteria walioko mdomoni wanaosababisha harufu mbaya ya kinywa, ni vizuri ukatumia limao baada ya kusafisha meno.

Hali kadhalika, malimao yana asid, ambayo ni chanzo kizuri cha vitamin C, ambayo ni nzuri kuzuia baridi na homa, lakini malimao pia husaidia kuzuia saratani ya damu.

Dk Mandai anabainisha kuwa pumu, malengelenge, uvimbe na vidonda pia vyote hivyo huweza kutatulika endapo mhusika atazingatia matumizi sahihi ya limao.

Pamoja na hayo, mtaalam huyo anasema kuwa maganda ya limao yanapotumika kwa kusgulia ngozi huwa ni dawa ya vipele, junjua na kuungua.

Pia maji ya limao huweza kuondoka makovu na mikunjo kwenye ngozi na kupunguza makovu makubwa kama ukinyunyizia kila mara. Hali kadhalika kutokana na uwezo wake wa kusafisha damu, maji ya limao huacha ngozi ikiwa inang’aa na yenye afya.

Hata hivyo, Dk Mandai anasema ni vizuri ukapata ushauri zaidi kutoka kwa wataam kabla ya kuamua kuanza kutumia limao kama tiba ili uweze kutumia kwa usahihi zaidi pasipo kuwa na madhara kwako. Pia unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic kituo kilichopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam utakutana na mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai na kupata suluhisho la magonjwa sugu.

No comments:

Post a Comment