Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 24 February 2015

ZIFAHAMU SABABU NA DALILI ZA TATIZO LA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI ( ANEMIA) SEHEMU YA (1)Anemia ni jina la jumla linalotumiwa kubainisha aina mbalimbali za upungufu wa damu mwilini.

Upungufu wa damu hujitokeza pale ambapo mkusanyiko wa pamoja wa chembe nyekundu za damu (haemoglobin)  zinapopungua kupita kiwango cha kawaida.

Mtu huweza kukubwa na tatizo hili la upungufu wa damu kutokana na sababu mbalimbali ikiwa hii ya kuvuja damu kunakotokana na jeraha au  kunakotokana na vipindi vya hedhi inayotoka kwa wingi sana.

Sababu nyingine inayoweza kusababisha tatizo hili ni uzalishwaji duni wa chembe nyekundu za damu unaosababishwa na upungufu wa vitamini au lishe duni na vile vile magonjwa sugu au ya muda mrefu ambapo bone marrow hushindwa kufana kazi inavyopaswa.

Mbali na sababu hizo sababu nyingine ni kuharibiwa kwa chembe nyekundu za damu kunakochangiwa na magonjwa ya kurithi.

Mara nyingi mtu mwenye tatizo hili la upungufu wa damu huonesha dalili za kuwa za kupauka mwili na hujisikia kuchoka, kuhisi kiu na kizunguzungu wakati anaposimama.

Dalili nyingine ni pamoja na kuhema isivyo kawaida na mpapatiko wa moyo wakati akitumia nguvu. 

Hilo ndio tatizo la upungufu wa damu mwilini pamoja na dalili zake, lakini nikusihi endelea kufuatilia tovuti hii (www.dkmandai.com) kila siku na kesho Mandaii Herbal Clini tutakufahamisha kuhusu aina za tatizo hili la upungufu wa damu na makundi gani huathirika zaidi pamoja na namna ya matibabu yake, tafadhali endelea kuwa nasi.

Sasa tupo tayari kuanza kupokea matangazo ya biashara yako yoyote na kukuwekea kwenye tovuti hii inayotembelewa na maelfu ya watu. Karibu sana gharama zetu ni nafuu sana piga simu namba 0758 163 818, 0672 060 006, Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment