Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 26 February 2015

ZIFAHAMU SABABU ZA TATIZO LA KUKOROMAJe, wewe ni miongoni mwa wale ambao wanakoroma usiku? Au wale ambao hulala kitanda kimoja na watu wenye tatizo hilo? Najua inawezekana ukawa kati ya sehemu moja kati ya hizo mbili.

Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene.

Tatizo hili mara nyingi huwapata zaidi watu wazima kuliko watoto. Hata hivyo hii si shida kubwa sana, lakini mara nyingi huleta tu karaha kwa mtu anayelala karibu na mkoromaji.

Tatizo hili hujitokeza pale mtu anapokuwa na kitu au sababu yoyote itakayoziba kuingia au kutoka kwa hewa mdomoni na katika pua. Hivyo kuta za koo hutikisika wakati wa kupumua na baadaye kusababisha kutoka kwa sauti inayosikika ya kukoroma.

Jambo la kuingia au kutoka kwa hewa huweza kuzuiwa na sababu mbalimbali kama ikiwemo hii ya kuziba tundu za pua kusiko kamili ambako husababisha nguvu zaidi kutumika katika kupitisha hewa kwenye pua wakati mtu akiwa amelala.

Miongoni mwa sababu zinazoweza kusababisha mtu kukoloma ni pamoja na kuwa na misuli dhaifu katika koo na ulimi. Suala hilo hutokea pale mtu anapolala fofofo au kuwa na usingizi mzito na kusababisha kukoroma.

Pia watu wanene pamoja na wazee huwa na nafasi kubwa ya kukabiliwa na tatizo hili
Hata hivyo wanaume ndio hukabiliwa zaidi na tatizo hili kuliko wanawake hii ni kutokana na wanaume kuwa na njia nyembamba zaidi ya hewa kuliko wanawake, lakini tatizo hili pia huweza kusababishwa na kurithi.


Madhara wanayoweza kuyapata watu wenye shida hii ni pamoja na kushindwa kulala vizuri yaani kuwa na usingizi wa mang’amung’amu, kutokana na hili mara nyingi watu hawa asubuhi huamka wakiwa wamechoka.

Ili kujua kama unatatizo hili ni lazima umshirikishe mwenzi wako au unayelala naye ili akuchunguze unapolala na kujua jinsi mwili wako unavyokuwa pale unapokoroma.

Unaweza kupunguza tatizo hili kawa kutokula mlo mkubwa kabla ya kulala, kutokunywa pombe kabla ya kulala pamoja na kutotumia vyakula au vinjwaji vyenye kafeini.

Vilevile wanaokoroma wanashauriwa kufanya mazoezi ya koo ambayo ni pamoja na kuimba na kusoma kwa kurudia rudia voweli (a,e,i,o,u) kwa nguvu kwa dakika kadhaa kwa siku.


Endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu basi wasiliana na Mandai Herbal Clinic kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.   

1 comment:

  1. Kwahiyo hakuna dawa za kumaliza tatizo hili mtaalamu

    ReplyDelete