Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 26 February 2015

ZINGATIA MAMBO HAYA ILI UWEZE KUISHI MAISHA MAREFU YENYE AFYA PIAHapa dunia kila mtu angependa kuishi maisha marefu tena yale ambayo hayana mateso mbalimbali yakiwemo ya magonjwa na hata yale ya kimaisha.


Lakini tunapozungumzia kuhusu muda wa kuishi hapa duniani mara nyingi huwa tunamuachia Mungu, hii ni kwa sababu tunaamini kuwa yeye pekee ndiye anayejua muda wa uhai au wa kuishi kwa binadamu yoyote hapa duniani.

Pamoja na hayo lakini ni vizuri tukafahamishana baadhi ya mambo machache ambayo kwa namna moja au nyingine huweza kukufanya pengine ukaishi maisha marefu zaidi hapa duniani

Mambo hayo ambayo yanaweza kuwa msaada kwako katika kukuongeza muda wa kuishi hapa duniani ni pamoja na kuhakikisha unakula lishe bora kila siku pamoja na kujenga utamaduni wa kupima afya yako mara kwa mara kadri uwezavyo na epuka matumizi ya pombe kupita kiasi.

Mengine ni kuepuka matumizi ya sigara, kuepuka unene kupita kiasi pamoja na kuhakikisha unakuwa ni mtu wa kufanya mazoezi mara kwa mara (kila siku)
Pia unapaswa kuepuka kutumia vyakula vyenye mafuta mengi, chumvi na sukari nyingi sambamba na kuepukana na msongo wa mawazo.

Mbali na hayo pia ni vizuri kuzingatia kula matunda na kunywa maji safi na salama ya kutosha kila siku, hali kadhalika hakikisha pia unaepuka matumizi ya dawa pasipo kupata ushauri wa wataalam wa afya.

Hayo ni mambo machache niliyoona ni vyema nikufahamishe msomji wetu wa tovuti hii, lakini kwa mambo mengine mengi unaweza kuendelea kuyapata endapo utakuwa karibu na tovuti hii kila siku.

Endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu basi wasiliana na Mandai Herbal Clinic kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.   

No comments:

Post a Comment