Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 28 March 2015

ANZA WEEKEND YAKO KWA KUTAZAMA PICHA HIZI ZA WADAU WETU KUTOKA KEKO MAGULUMBASI


Mandai Herbal Clinic pamoja na Mandai Entertainment kwa kushirikiana na Uhuru Fm kila Ijumaa hutembelea sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa lengo la kushare na wananchi  husika kuhusu huduma za Mandai Herbal Clinic na Mandai Entertainment pamoja na masuala ya mtaa husika kwa ujumla, huku tukitoa zawadi mbalimbali zikiwemo T.shirt na vitabu vya afya.

Ijumaa ya Marchi 27 tulikuwa maeneo ya Keko Magulumbasi na kujumuika pamoja na wananchi wa eneo hilo, hivyo nimeona ni vyema nikupe hizi picha chache za wananchi wa keko pale walipoamua kutokea mbele ya kamera yetu
Hawa ni miongoni mwa wale walioweza kujibu maswali yetu vizuri na hivyo tuliwatunuku T.shirt kama unavyoona wakiwa wameng'aa tayari

Kulia ni Mc Jojoo ambaye ni Mtangazaji wa Redio Uhuru Fm kupitia kipindi cha Tashititi zetu akiwa sambamba na wadau wakionesha maandishi ya nyuma ya T.shirt zao


Wadau wakiwa na nyuso za furaha (katikati mwenye nguo nyekundu ni Mc Jojoo kutoka Uhuru Fm) ambaye ni moja ya timu yetu ambaye huongozana nasi kila siku ya Ijumaa katika zoezi hilo, huku akiwa na wajibu wa kutuunganishwa live kwenye kipindi cha taarabu (Tashititi zetu) cha Redio Uhuru

Mtangazaji wa Redio Uhuru Fm Mc Jojoo akimhoji binti huyu kutaka kujua ni kwa kiasi gani anafahamu kuhusu Mandai Entertainment

Mc Jojoo akimhoji pia jamaa huyu kuhusu Mandai Herbal ClinicHuenda wiki Ijayo tutakuwa mtaani kwako kaa tayari kutupokea na tutakuja mengi kuhusu Mandai Herbal Clinic na Mandai Entertainment, lakini na wewe pia utatujuza yako kutoka hapo mtaani kwako ambayo yatakuwa yakisikika live kupitia Redio Uhuru Fm. Pia tunasema asanteni sana wakazi wa Keko Magulumbasi kwa kutupokea mtaani kwenu.

No comments:

Post a Comment