Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 10 March 2015

BORESHA AFYA YA NYWELE ZAKO KWA KUTUMIA VYAKULA NA MATUNDAMara nyingi kina mama na kina dada hupenda kuonekana warembo hususani katika masuala ya nywele, hapo ndipo utasikia wakijinadi kuwa, ‘mwanamke nywele bwana.’


Lakini ili kuwa na nywele nzuri na zenye afya huhitaji matunzo sambamba na namna mhusika anavyoishi ‘life style’ ikiwemo masuala ya mpangilio wa vyakula.

Vifuatavyo ni baadhi ya vyakula ambavyo mhusika anapokula huweza kumsaidia sana katika kumfanya kuwa na afya njema ya nywele zake.

Ili kuwa na nywele nzuri na zenye afya mwili huhitaji kuwa na protini, ni vizuri ukahakikisha kuwa unakula mlo wenye protini aambao utasaidia kuwa na nywele zenye afya.

Endapo mtu atakosa protini nywele huwa kavu na huweza kuchangia nywele kukatika ovyo.

Vyakula vya protini ni pamoja na mayai, maziwa, kuku, maharage pamoja na baadhi ya vyakula jamii ya karanga.

Madini ya chuma ni muhimu pia katika kutunza nywele, mtu anapokosa madini chuma husababisha kuathiri mzunguko wa ukuaji wa nywele. Madini haya huweza kupatikana kupitia ulaji wa nyama. Hali kadhalika ulaji wa mboga za majani mfano spinachi husaidia mtu kupata madini haya .

Kirutubisho kiingine ambacho ni muhimu kwa afya ya nywele zako ni uwepo wa vitamin C za kutosha mwilini, hii unaweza kuipata kwa kupendelea kula matunda kama vile machungwa, mapapai pamoja na viazi vitamu.

Vitamin A pia ni muhimu katika kutunza afya ya nywele zako na inahitajika mwilini katika kusaidia kutengeneza malighafi iitwayo sebum ambayo ni kama mfano wa mafuta maalum ambayo hutolewa na mwili na kazi yake ni kuifanya ngozi na nywele kutopauka.

Vitamini A huweza kupatikana kwa kula karoti, maboga pamoja na viazi vitamu.

Jua pia huathiri afya ya nywele pamoja na ngozi kwa ujumla, hivyo ni vyema kuhakikisha unatumia vyakula ambavyo vimesheheni vitamin E ambavyo vitasaidia sana kulinda afya ya nywele zako pia. Mfano wa vyakula ambavyo vitaweza kukupatia vitamin hiyo ni pamoja na karanga.

Pamoja na hayo, unaweza kutumia njia hii kwa kufanya nywele zako kuwa nzuri zaidi chukuwa kiini cha yai kisha changanya na mchanganyiko wa parachichi pamoja na asali kijiko kimoja kisha tumia mchanganyiko huo kwa kupaka kwenye nywele zako vizuri na ukae na mchanganyiko huo kwa muda wa nusu saa kisha osha nywele zako kwa maji safi. Hii itasaidia kufanya nywele zako kuonekana vizuri na kuwa zenye afya zaidi.


Mandai Herbal Clinic inaendelea kukukumbusha kwamba endapo unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu unaweza kufika kituoni kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata suluhisho la matatizo yako. Pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.  


No comments:

Post a Comment