Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 31 March 2015

DK AMOS YOYO ATEMBELEA MANDAI HERBAL CLINIC NA KUZUNGUMZIA NAMNA LIMAO LINAVYOWEZA KUWASAIDIA WANAWAKEBaadhi ya kinamama na wanawake wamekuwa wakikosa raha na kupata shida na wakati mwingine huhisi maumivu wakati wanapokuwa katika siku zao yaani hedhi.


Hata hivyo kuna baadhi ya kinamama wao hujikuta wakitokwa na damu nyingi zaidi kuliko ilivyo kawaida wakati wanapokuwa katika hedhi jambo ambalo huwakwaza kinadada na wanawake wengi kwa ujumla na mara nyingine kupelekea hata kushindwa kufanya shughuli zao za kila siku.

Lakini wiki hii Mandai Herbal Clinic ilipata nafasi ya kutembelewa na mmoja wa matabibu wa tiba asili kutoka Life Style Clinic, Dk Amos Yoyo ambaye alipata nafasi pia ya kuzungumza na kitengo chetu cha habari kutoka Mandai Herbal Clinic na moja ya mambo aliyoamua kushare nasi ni hili tatizo la kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi na kuelezea ni namna gani unaweza kukabiliana nalo.

Dk, Yoyo kwanza anasema ni kweli baadhi ya wanawake wamekuwa wakikabiliwa na tatizo hilo na kuwafanya kukosa raha kila inapofika wakati wa siku zao (hedhi) na mara nyingine hulazimika kabisa kusitisha hata shughuli zao pale wanapokuwa katika hali hiyo.

Hata hivyo, Dk Yoyo anasema kwamba moja ya njia inayoweza kusaidia katika kukabiliana na tatizo hilo ni pamoja na matumizi ya limao au ndimu.

“Tunashauri mtu kutumia ndimu au limao kwani ni tiba kubwa sana ambayo ina vitamin C kwa wingi” alisema Dk Yoyo.
Limao linaloelezwa kuwa tiba


Akifafanua kuhusu namna ya kutumia limao/ ndimu kama tiba Dk Yoyo anasema kuwa, mhusika anapaswa kutumia ndimu asilia ambapo mhusika atatakiwa kukamua ndimu tatu na kunywa kutwa mara mbili ndani ya kipindi cha siku tatu.
 
Dk Abdallah Mandai (kulia) akizungumza na Dk Amos Yoyo kuhusu masuala ya taaluma yao wakiwa katika moja ya sehemu za kurekodia vipindi katika ofisi za Mandai Entertainment (Mandai Studio)
Mbali na hayo Dk Yoyo pia alitumia fursa hiyo kumshukuru Dk Abdallah Mandai ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mandai Herbal Clinic kwa kuanzisha utaratibu wa kutembeleana na kusema kuwa wanapotembelea husaidia sana kubadilishana ujuzi mbalimbali katika taaluma hiyo.

Pamoja na hayo aliwataka Watanzania kuendelea kuziamini tiba asilia kutokana na tiba hizo kwa sasa kutumia vifaa vingi vya kisasa vyenye uwezo mkubwa katika kutambua magonjwa mbalimbali.

“Tiba asili tunayofanya sisi wengi wanaiamini kwasababu hakuna lamri na tunatumia vifaa vya kisasa” alisema Dk Yoyo.

Dk Amos Yoyo anapatikana katika kliniki yake iitwayo Life Style Clinic inayopatikana maeneo ya Malapa jijini Dar es Salaam mkabala na ofisi za Star Times. Au unaweza kuwasiliana naye kwa simu namba 0713 999 255, 0786 523028

No comments:

Post a Comment