Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 14 March 2015

DK RUSIGWA WA SURE HURBAL CLINIC ATEMBELEA MANDAI HERBAL CLINIC

Tabibu Lusigwa(kulia) wa Sure Herbal Clinic akizungumza mawili matatu na Dk Abdallaha Mandai
Mtaalam wa tiba asili nchini na Mkurugenzi  Mkuu wa kituo cha Sure Hurbal Clinic, Tabibu Lusigwa Ijumaa hii alitembelea  kituo cha Mandai Herbal Clinic kwa lengo la kuangalia utanuzi wa kituo hicho sambamba na kubadilishana mawazo na Dk Abdallaha Mandai juu ya taaluma yao hiyo.
Akizungumza na kitengo cha habari cha Mandai Herbal Clinic, Tabibu Lusigwa alisema kwamba imekuwa ni nadra sana katika taaluma yao hiyo kutembeleana na kujuliana hali pamoja na kubadilishana ujuzi kuhusu kazi zao, lakini kwake tabibu Lusigwa amesema amekuwa akipenda kujua mengi na kushirikiana na matabibu wenzake pale anapopata nafasi hiyo.

"Ujue Mungu alitupatie masikio kwa lengo la kusikia na kuingiza vitu na ndio maana mimi hupenda kushirikiana na matabibu wenzangu ambao wapo tayari ili nisikie mengi na tubadilishane mawazo kwa lengo la kusogeza mbele taaluma yetu hii na kuhakikisha tunaendelea kutoa tiba kwa umma wa Watanzania" alisema tabibu Lusigwa.

Aidha, tabibu Lusigwa aliongeza kwa kusema kuwa yeye haoni haja ya kujengeana chuki kati yao matabibu na badala yake akashauri ni vyema wakashirikiana kwa dhati.

Naye Dk, Abdallah Mandai ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mandai Herbal Clinic alionekana kufurahia ujio wa tabibu Lusigwa kituoni hapo, huku akisema kuwa tabibu Lusigwa amekuwa akishirikiana naye kwa muda mrefu sasa na wamekuwa wakishauriana mambo mengi kuhusu taalam yao hiyo. 

Mbali na hayo naye Dk, Mandai aliwataka matabibu kujenga tabia ya kushirikiana zaidi kwa lengo la kuweza kuifikisha mbali zaidi taaluma hiyo.

"Mimi nadhani tungekuwa tunashirikiana huenda tungekuwa mbali zaidi katika taaluma hii, na hakuna haja ya kuchukiana kikubwa ukiona mwenzio anafanikiwa unapaswa kujenga kumfuata na kumuomba ushauri ili na wewe uweze kufika mbali zaidi." alisema Dk, Mandai.

No comments:

Post a Comment