Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Sunday, 22 March 2015

DK MANDAI WEEKEND HII ANAKUPATIA SABABU HIZI ZINAZOWEZA KUCHANGIA MWANAMKE KUTOSHIKA MIMBA


Tatizo la mwanamke kushindwa kushika mimba husababishwa na sababu mbalimbali hapa leo nitazungumzia baadhi ya sababu hizo zinazoweza kuchangia mwanamke kushindwa kushika mimba.


Tatizo hili tunaweza kuliweka katika makundi mawili yaani ‘primary Infertility’ ambapo mwanamke anakuwa hana historia ya kupata ujauzito, lakini pili kundi la secondary infertility’, hapa mwanamke ankuwa alishawahi kupata ujauzito pasipo kujalisha kama alijifungua au iliharibika.

Tatizo hili la mwanamke kushindwa kupata mimba kitaalam huitwa ‘infertility’ au ugumba.

Sababu inayoweza kuchangia tatizo hili ni pamoja na upevushaji wa mayai ‘Ovulatory’. Tatizo hili huathiri wanawake kwa kiasi kikubwa ambapo mwanamke hupata siku zake kama kawaida lakini hapevushi mayai. Hali hii husababisha na matatizo katika mfumo wa homoni mwilini.

Tatizo hili huweza kutokea kutokana na mabadiliko ya mwilini au matumizi yanayohusiana na dawa za homoni kutumika kiholela au matumizi ya baadhi ya vyakula au vipodozi.

Sababu nyingine ni maambukizi katika viungo vya uzazi, na wakati mwingine huweza kuchangiwa hata na lishe duni kwa mwanamke husika.

Pia utoaji wa mimba, maambukizi ya mara kwa mara ukeni husababisha athari katika kizazi na mirija hivyo usababisha ugumba kwa kiasi kikubwa.

Aidha, mwanamke pia anaweza kuwa na kasoro katika tabaka la ndani la kizazi ambapo hutoka kwa nje badala kuwa ndani. Hali hii kitaalam inaitwa ‘Endometriosis’.  Ingawaje hili siyo tatizo linalojitokeza kwa ukubwa sana lakini huathiri baadhi ya wanawake. Mwanamke mwenye tatizo hili hulalamika maumivu chini ya tumbo na huwa na maumivu makali wakati wa hedhi na kusababisha damu ya hedhi kutoka kidogo kidogo.

Ni wazi kwamba matatizo ya ugumba ni makubwa na huumiza vichwa vya watu wanaotafuta ujauzito. Hata hivyo ni vizuri kufanya uchunguzi kwa madaktari wa magonjwa ya kinamama na matatizo ya uzazi katika hospitali za mikoa na wilaya. 

Pia unaweza kufika Mandai Herbal Clinic na kuonana nasi ili tuweza kuona namna ya kukusaidia kliniki yetu ipo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment