Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 11 March 2015

ENDELEA KUFAHAMU KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO (2)

Baada ya jana March 10 kuanza kuzungumzia kuhusu vidonda vya tumbo, leo tena tunaendelea ambapo tutaanza kuangalia kuhusu dalili za vidonda vya tumbo.


Mara nyingi kuhusu dalili za vidonda vya tumbo huwa hakuna dalili za moja kwa moja, lakini mara nyingi huenda mhusika akapata ishara zifuatazo.

Miongoni mwa ishara hizo ni pamoja na kuhisi maumivu makali ya tumbo kwa muda mrefu hususani pale ambapo mhusika anakuwa hajapata chakula.

Aidha, dalili nyingine ni kutapika mara kwa mara, kukosa hamu ya kula, kupungua uzito, mwili kukosa nguvu, tumbo kujaa gesi na inapofikia hatua mbaya zaidi basi mhusika huweza kuanza kutapika damu.

Kuna madhara kadhaa ambayo huweza kujitokeza kutokana vidonda vya tumbo ambayo ni pamoja na kulika kwa utumbo hali inayoweza kuvilia kwa damu kwa ndani.
Pia madhara mengine ni kushuka kwa uwezo wa kufanya kazi kwa ufasaha, lakini wanaume pia huweza kupunguza uwezo wao kufanya tendo la ndoa.

Mambo yanayoweza kukusaidia katika kuepuka tatizo hili la vidonda vya tumbo ni pamoja na kuepuka matumizi ya sigara na tumbaku. Sigara na tumbaku zina kemikali inayoitwa nicotine ambayo inauwezo wa kusababisha vidonda vya tumbo. Tafiti zimekuwa zikionesha kwamba watumiaji wa sigara na tumbaku huwa katika hatari zaidi ya kupata vidonda vya tumbo.

Pamoja na hayo, ili kuepukana na ugonjwa huu unapaswa kuzingatia kula mlo kamili tena kwa wakti muafaka.

Epuka kuwa na msongo wa mawazo hii pia ni moja ya sababu inayochangia tatizo la vidonda vya tumbo.

Baada ya kuyafahamu hayo nikusihi endelea kuwa karibu na tovuti hii ambapo kesho nitakuletea namna ya kutumia tiba asili katika kutibu vidonda vya tumbo.Mandai Herbal Clinic inaendelea kukukumbusha kwamba endapo unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu unaweza kufika kituoni kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata suluhisho la matatizo yako. Pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.  

No comments:

Post a Comment