Thursday, 19 March 2015

FAHAMU AINA HIZI 6 ZA JUISI NA FAIDA ZAKE MWILINILeo ninayofuraha ya kukufahamisha aina za juisi za matunda na faida zake mwilini katika kutibu magonjwa au kutoa kunga dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Kumbuka kuna ule usemi usema chakula ni dawa, na kumbuka kwamba chakula unachokula leo ndicho ambacho huamua hali ya afya yako ya kesho.

Unaweza kuishi maisha marefu au bila kuugua endapo utazingatia kula vyakula muhimu katika kila mlo wako hivyo ni vyema kuzingatia milo yetu ya kila siku.

CHUNGWA, TANGAWIZI NA TANGO
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya husaidia kung’arisha ngozi na kuifanya kuonekana laini, huku pia ikisaidia kupunguza joto la mwili, lakini kwa wale wenye shida ya kuwa na ngozi kavu juisi hii huwasaidia sana.

KAROTI, TUFAHA NA TANGAWIZI
Mchanganyiko wa matunda haya hutoa juisi ambayo huwa na uwezo wa kuondoa sumu mwilini na kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Tufani ni Apple kwa kiingereza. 

NDIZI, NANASI NA MAZIWA
Hii ni juisi yenye kiasi kingi cha vitamin na virutubisho mbalimbali vyenye faida mwilini, huku ikisaidia sana kuzuia tatizo la ukosefu wa choo.

KAROTI, EMBE, TUFAHA NA PEASI
Juisi hii inaelezwa kusaidia kuzuia athari ya sumu mwilini na hupunguza shinikizo la dmau na kuondoa mlundikano wa uchafu mwilini.

PEASI NA NDIZI
Juisi hii husaidia kurekebisha kiwango cha sukari katika damu na huwafaa zaidi wagonjwa wa kisukari.

NANASI, TIKITI MAJI NA TUFAHA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya kazi ya kuondoa chumvi nyingi mwilini na husafisha kibofu cha mkojo pamoja na figo. Hivyo juisi hii ni nzuri kwa wale wenye matatizo ya kibofu na figo na hata kujikinga na magonjwa hayo.

Hata hivyo, pamoja na juisi hizo kuwa na manufaa mwilini pia unapaswa kuzingatia usafi wa matunda yanayotumika na usafi wakati wa matayarisho, huku matunda yakiwa ni yale yaliyoiva vizuri.

Pia zingatia kuweka sukari kiasi kidogo sana kuliko kuweka sukari nyingi maana huweza kuwa na madhara kiafya pia.

Leo ninayofuraha ya kukufahamisha aina za juisi za matunda na faida zake mwilini katika kutibu magonjwa au kutoa kunga dhidi ya magonjwa mbalimbali
Kumbuka kuna ule usemi usema chakula ni dawa, na kumbuka kwamba chakula unachokula leo ndicho ambacho huamua hali ya afya yako ya kesho.
Unaweza kuishi maisha marefu au bila kuugua endapo utazingatia kula vyakula muhimu katika kila mlo wako hivyo ni vyema kuzingatia milo yetu ya kila siku.
CHUNGWA, TANGAWIZI NA TANGO
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya husaidia kung’arisha ngozi na kuifanya kuonekana laini, huku pia ikisaidia kupunguza joto la mwili, lakini kwa wale wenye shida ya kuwa na ngozi kavu juisi hii huwasaidia sana.
KAROTI, TUFAHA NA TANGAWIZI
Mchanganyiko wa matunda haya hutoa juisi ambayo huwa na uwezo wa kuondoa sumu mwilini na kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Tufani ni Apple kwa kiingereza.
NDIZI, NANASI NA MAZIWA
Hii ni juisi yenye kiasi kingi cha vitamin na virutubisho mbalimbali vyenye faida mwilini, huku ikisaidia sana kuzuia tatizo la ukosefu wa choo
KAROTI, EMBE, TUFAHA NA PEASI
Juisi hii inaelezwa kusaidia kuzuia athari ya sumu mwilini na hupunguza shinikizo la dmau na kuondoa mlundikano wa uchafu mwilini.
PEASI NA NDIZI
Juisi hii husaidia kurekebisha kiwango cha sukari katika damu na huwafaa zaidi wagonjwa wa kisukari.
NANASI, TIKITI MAJI NA TUFAHA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya kazi ya kuondoa chumvi nyingi mwilini na husafisha kibofu cha mkojo pamoja na figo. Hivyo juisi hii ni nzuri kwa wale wenye matatizo ya kibofu na figo na hata kujikinga na magonjwa hayo.

Hata hivyo pamoja na juisi hizo kuwa na manufaa mwilini pia unapaswa kuzingatia usafi wa matunda yanayotumika na usafi wakati wa matayarisho, huku matunda yakiwa ni yale yaliyoiva vizuri.

Pia zingatia kuweka sukari kiasi kidogo sana kuliko kuweka sukari nyingi maana huweza kuwa na madhara kiafya pia.

Endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu fika Mandai Herbal Clinic au wasiliana na Dk Mandai kwa simu namba, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.  

No comments:

Post a Comment