Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 13 March 2015

FAHAMU MAGONJWA AMBAYO HUPASWI KUYAPUUZABinadamu mwenye afya njema huwa na kinga kwa ajili ya kupambana na maradhi mbalimbali.


Mara nyingine kinga za mwili hushindwa kupambana na magonjwa ambayo ni hatari sana hivyo huhitaji tiba au msaada wa kukabiliana utakaokuwezesha na ugonjwa huo. 

Leo nimeona ni vyema tukafahamishana kuhusu magonjwa haya ambayo haupaswi kuyapuuza mara unapoyapata.

MALENGELENGE
Huu ni ugonjwa hatari sana ambao husababishwa na aina mbili za virusi (HSV-1 na HSV-2) na huambatana na dalili kama homa kali, kutapika, vipele au vidonda sehemu za siri na mdomoni. Ugonjwa huu usipopata tiba mapema husababisha virusi hawa kuharibu mishipa ya damu na kusabababisha kifo.

MAFUA MAKALI
 Ugonjwa huu wengi huwa wanaupuuza, na husababishwa na virusi viitwavyo influenza A, B na C na usipotibiwa mapema huaribu mfumo wa upumuaji na kusababisha kifo.

KIPINDUPINDU
Ni ugonjwa wa mlipuko ambao ni hatari sana kwa kupoteza maisha ya watu wengi kutokana na upungufu wa maji mwili unaosababishwa na kuharisha pamoja na kutapika.

MALARIA
Malaria ni ugonjwa hatari sana kwani huathiri mzunguko wa damu, ini na mfumo wa fahamu kwa kasi zaidi.


KUPOOZA
Ugonjwa huu husababishwa na kupooza kwa mishipa ya fahamu katika ubongo na uti wa mgongo na kusababisha ulemavu wa viungo na hata kupelekea kifo.

 KISUKARI
Ugonjwa huu ni vigumu kuugundua mapema na hivyo uendelee kusababisha madhara mpaka pale unapogundulika huwa katika hatua mbaya inayosababisha magonjwa ya moyo, figo, upofu na hata kukatwa miguu.

PUMU
Ugonjwa huu ni hatari na humfanya kupatwa na mtu kupatwa na aleji ya vitu mbalimbali, huku ikiharibu mfumo wa upumuaji kutokana na kuvimba na kuziba kwa njia ya hewa, kukooa, maumivu makali ya kifua na kushindwa kupumua.

MAGONJWA YA MOYO
Magonjwa ya moyo husababisha vifo vingi pale moyo na mishipa ya damu inaposhindwa kupeleka damu na hewa ya kutosha kwenye ubongo na sehemu mbalimbali za mwili.

UKIMWI
Ugonjwa huu unaingia kwenye orodha hii kutokana na kukosa tiba ya moja kwa moja zaidi ya kufifisha tu makali. Mtu huweza kupata ugonjwa huu kupitia vitu vyenye ncha kali, kufanya mapenzi bila kinga au kupitia kwa mama kwenda kwa mtoto endapo mama atakuwa hajazingatia taratibu za kiafya kipindi cha ujauzito wake.

Endapo unatatizo lolote la kiafya unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 3682 442, Barua pepe ni dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kufika Mandai Herbal Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment