Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 4 March 2015

FAHAMU VYAKULA VITAKAVYOKUONDOLEA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA

Baadhi ya watu wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa na kuwafanya wengi wao kukosa amani na raha hata katika maisha yao na wenzi wao.


Mandai Herbal Clinic leo tunakusogezea karibu baadhi ya vyakula ambavyo utaweza kutumia na vikakusaidia katika kuondokana na tatizo hilo.

Miongoni mwa vyakula hivyo ni pamoja na vyakula vya nafaka ambavyo huwa na nyuzinyuzi (fiber) na sukari ngumu (complex sugar) ambavyo husaidia kutunza uzito wa mwili.

Pia vyakula hivi vya nafaka husaidia katika kuzalisha homoni za testosterone kwenye damu, huku vikimuwezesha mtu kuwa na nguvu hatimaye kuweza kushiriki vizuri tendo.

Pilipili pia huweza kusaidia kumpatia mtu hamu ya kushiriki tendo hii ni kwa sababu pilipili inauwezo kusisimua mfumo wa ufahamu (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo huwezesha kumshwa hisia kwa haraka.Aidha, mlo wenye matunda na mboga za majani nao una nafasi kubwa katika kuongeza hamu ya tendo la ndoa. Pia matunda na mboga za majani hupunguza kiwango cha mafuta na unene (cholesterol), kuongezeka kwa mafuta mwilini huzuia mzunguko wa damu kwa kubana mishipa ya damu.  Wanandoa wanapozidi kunenepeana hupelekea hata hamu ya tendo la ndoa kupungua.Tangawizi pia husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, na tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume. Inaweza kuliwa mbichi, au kupikwa au kuanikwa na kuwa kama unga.Mbali na vyakula hivyo pia karanga huhusika moja kwa moja na kutunza mfumo wa mzunguko wa damu. Kwa kawaida mfumo wenye afya (mzunguko wa damu) katika uke na uume huwezesha mwanaume na mwanamke kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa zuri.

Pia karanga zina madini muhimu kama vile magnesium, asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika usalishaji wa mbegu za mwanaume.No comments:

Post a Comment