Tuesday, 31 March 2015

HAPA KUNA VITU 7 MUHIMU KWA AJILI YA AFYA BORA ZIPO PIA MBOGA ZA MAJANI

Kuna mambo mengi ambayo huchangia mtu kuwa na afya bora, mbali ya chakula pia namna unavyowaza na kufikiri huchangia afya kuwa bora au laa!.


Moja ya mambo ambayo ni muhimu katika kuchangia kuwa na afya bora ni pamoja na haya yafuatayo:

Kupata nafasi ya kulala kiasi cha kutosha, usingizi ni sehemu muhimu sana katika afya. Mbali ya kuwa usingizi huwa na faida kwa ajili ya afya ya akili/ubongo wetu, lakini pia ni muhimu kwa miili yetu.Afya njema huambatana na mapumziko kwani husaidia mwilii kujijenga zaidi.
 
Kunywa Maji kwa wingi, maji ni kitu muhimu sana kwa afya zetu. Asilimia 60% ya miili yetu imetengenezwa au imesheheni maji. Maji yanahitajika kwa ajili ya kuondoa takataka au vitu visivyofaa kutoka mwilini. Hali kadhalika maji ndio hubeba virutubisho na oxygen.

Unaweza kujichunguza endapo mwili wako una maji ya kutosha kwa kuangalia mkojo wako. Mkojo wako unatakiwa kutokuwa na rangi (colorless) au kuwa wa njano kidoogo. Tofauti na hapo ni ishara kwamba hauna maji ya kutosha mwilini. Pia unaweza kutambua kama hauna maji ya kutosha pale unapoona unakaukwa na midomo (lips) na hata ulimi na pia kupata kiasi kidogo cha mkojo.

Fanya Mazoezi, fanya mazoezi angalau mara tatu katika wiki, ni vyema pia ukatenga muda wa kutembea japo kwa dakika 30. Muhimu zaidi ni kuchagua aina ya mazoezi unayoyaoenda. Kimsingi mazoezi ni muhimu kwa kila mtu.

Tumia matunda kwa wingi, hii ni kwa sababu matunda ni chanzo kizuri zha madini na vitamins ambazo miili yetu huhitaji sana kwa ajili ya afya bora. Mfano kama machungwa yamesheheni faida kubwa zaidi kiafya kuliko vidonge vya Vitamin C. Aina nyingine za matunda muhimu kwa afya ni pamoja na Parachichi (Avocado), matikiti maji, apple, zabibu, mapapai nk.

Kula mboga za majani, mboga za majani (vegetables) ni muhimu sana kwa afya zetu. Jitahidi kupata angalau zaidi ya aina 5 za mboga za majani.

Punguza Kula Vyakula vya Viwandani, Jitahidi kuviepuka vyakula hivyo kwa kadri unavyoweza.Mara nyingi vyakula vya makopo huwa na ‘ingredients’ ambazo hazifai kwa afya zetu. Kwa mfano,vingi miongoni mwa vyakula hivyo huwa na chumvi nyingi kitu ambacho ni chanzo maradhi ya moyo. Unaposhindwa kabisa kujizuia kununua vyakula hivyo vya viwandani/makopo basi jaribu kuangalia ambavyo havina sukari au chumvi.

Jipende, Njia mojawapo ya kupata afya bora ni hii ya kujipenda. Hii inamaanisha kujithamini kwa kujiepusha na mambo mbalimbali ambayo huweza kuhatarisha afya yako kama vile uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe kupindukia nk.


Kama unasumbuliwa na magonjwa sugu pia unaweza fika Mandai Herbal Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaa. Au wasiliana na Dk Mandai kwa namba za simu zifuatazo  0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443


No comments:

Post a Comment