Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 16 March 2015

HAYA NDIYO ALIYOSHARE NASISI TABIBU RUSIGWA KUTOKA SURE HURBAL CLINIC KUHUSU HILI LA KULEGEA KWA MISULI YA UKEHivi karibuni Tabibu Rusigwa alitembelea Mandai Herbal Clinic na kukutana na kitengo cha habari kutoka Mandai Herbal Clinic na kuzungumzia kuhusu tatizo la kulegea kwa misuli ya uke yaani (vaginal prolapsed).


Tabibu Rusigwa ambaye ni Mkurugenzi wa Sure Hurbal Clinic anasema kuwa tatizo hili huwatokea zaidi wanawake walio katika umri mkubwa ingawa pia linaweza kutokea katika umri mdogo.

“Tunapozungumzia kulegea kwa misuli ya uke hapa kuna tofauti kidogo na kutanuka kwa misuli hiyo.Tukizungumzia kulegea ina maana misuli ya ukeni inashindwa kubana na kuachia njia.Hapa misuli inayoachia njia inapolegea hata ukichuchumaa uhisi nyama zimejaa ukeni.” Alisema Tabibu Rusigwa.

Chanzo cha tatizo
Aidha, tabibu huyo alibainisha kuwa kulegea kwa misuli ya uke hutokana na matatizo mbalimbali na hasa uzazi wa karibu karibu.

“Mama anayezaa kwa vipindi viwili vifupi vifupi kwa njia ya kawaida hupatwa na tatizo hili, kulegea kutokana na matatizo ya vichocheo (Hormones) za kike, kulegea kunaweza kusababishwa na magonjwa sugu kama kansa,TB na maambukizi ya HIV au magonjwa ya zinaa haswa kawende” alisema Tabibu Lusigwa.

Mbali na hayo, tabibu Rusigwa aliongeza kwamba “mama anayeongezwa njia, baada ya uke kutanuka pia misuli pia inalegea, ingawa uke pia unaweza kutanuka hata bila hata ya misuli kulegea.Tatizo hili la kulegea misuli pia huchangiwa na umri mkubwa kwahiyo kwa wabibi hali hii inapojitokeza ni kawaida hasa kuanzia umri wa miaka 70 na kuendelea”

Dalili za tatizo
Tabibu huyo anaeleza kwamba mama mwenye tatizo hili wakati wa kujisafisha ukeni huhisi kama tundu limeziba au limejaa nyama na humlazimu kutumia muda kujisafisha mara kwa mara atakuwa anasumbuliwa na muwasho na uchafu wa mara kwa mara wakati wa kufanya tendo la ndoa, maumivu wakati wa tendo la ndoa ambayo hutokea pale tu inapotokea michubuko na maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Mama mwenye tatizo hili wakati wa kujisafisha ukeni atahisi kama tundu limeziba au limejaa nyama na inabodi atumie muda kujisafisha mara kwa mara atakuwa anasumbuliwa na muasho na uchafu wa mara kwa mara wakati wa kufanya tendo la ndoa, maumivu wakati wa tendo la ndoa ambayo hutokea pale tu inapotokea michubuko na maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Namna ya uchunguzaji wa tatizo hili

Aidha, tatizo hili huambatana na uambukizo wa muda mrefu ukeni, pamoja na mama kutofurahia tendo la ndoa, hali kadhalika uambukizi huweza kupanda hadi kwenye mlango wa uzazi,tumbo la uzazi, mirija na vifuko vyo mayai.

Maambukizo yanapofikia huko mama huumwa na tumbo chini ya kitovu mara kwa mara  pamoja na mwenendo wa siku za hedhi kuvurugika.

Tabibu Rusigwa aliendelea kusema kuwa, hali ya kulegea kwa misuli ya uke pia humuathiri hata mume kwani naye hushindwa kufurahia tendo la ndoa, kulegea na kutanuka kwa uke yote huathiri mahusiano ya kimapenzi kwani mama hafurahii na baba yake hafurahii tendo la ndoa.

Katika kutanuka kwa uke tumeona kuwa uke unatanuka zaidi ya kipenyo chake cha halali ambacho ni sentimeta nne,hivyohivyo kipenyo cha uume ni sentimeta nne.

Endelea kuwa karibu na tovuti hii ya www.dkmandai.com ambapo kesho Marchi 17 nitamalizia kuhusu mada hii kwa kuendelea kukuletea mahojiani yetu na Tabibu Rusigwa ambapo atamalizia namna ya kutambua tatizo hili na matibabu yake.


Mandai Herbal Clinic inaendelea kukukumbusha kwamba endapo unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu unaweza kufika kituoni kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata suluhisho la matatizo yako. Pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment