Monday, 23 March 2015

HAYA NI VYEMA YAKAZINGATIWA KWA MAMA MJAMZITO
Mwanamke anapokuwa mjamzito anapaswa kula chakula chenye virutubisho vya kutosha pamoja na madini ya chuma, hii ni kwa sababu madini hayo ya chuma husaidia ongezeko la damu mwilini hivyo kumsaidia mwanamke pale anapokuwa amepoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.


Aidha, mama mjamzito pia anapaswa kuepuka maambukizo katika mlango wa kizazi na sehemu za siri na pale inapotokea akapata maambukizi kama hayo ni vyema akapata matibabu sahihi mapema zaidi.

Mama mjamzito anapaswa kuepuka matumizi ya pombe na dawa za kulevya, matumizi ya vilevi hivyo huhatarisha afya ya mtoto na huweza kuchangia mtoto kuzaliwa akiwa na ulemavu, hivyo wataalam wa afya hupendekeza mama mjamzito asinywe pombe hata kwa kiwango kidogo.


Mama mjamzito hupaswa kuepuka kutumia dawa ovyo pasipo maelekezo maalum ya daktari 

Mbali na hayo, pia mama mjamzito anatakiwa kuepuka kuwa na uzito kupita kiasi pamoja na kuzingatia usafi wake binafsi ambao ni wa kawaida tu kama vile kudumisha kunawa mikono na kuosha vyakula kabla ya kula

Endapo unasumbuliwa na magonjwa sugu fika Mandai Herbal Clinic au wasiliana na Dk Mandai kwa simu namba, 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment