Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 30 March 2015

HII NI MAALUM KWA WEWE MZAZI AMBAYE UNAAMINI KUWA KUNENEPA KWA MTOTO NDIO KUWA NA AFYA BORA
Suala la kunenepa kupita kiasi ni moja ya tatizo ambalo linaonekana kupuuzwa na wazazi walio wengi, licha ya kuonekana kwa dalili za mapema kuwa watoto wao wamenenepa kupita kiasi.


Hata hivyo madaktari wanasema kuwa wazazi wengi hawajui madhara ya afya kwa watoto walionenepa kupita kiasi.

Katika utafiti uliofanyika hivi karibuni na kujumuisha zaidi ya familia 2,976 nchini Uingereza ni wazazi 4 pekee waliokuwa na shauku kuwa mtoto wao alikuwa amenenepa kupita kiasi. Huku madaktari wenyewe wao walikuwa wamewatambua watoto 369 kati yao waliokuwa na kiwango cha juu cha mafuta mwilini.

Kulingana na takwimu hizo zinaonesha kuwa watoto walionenepa kupita kiasi sasa wamekuwa kawaida tu majumbani, huku watafiti hao wakionya kuwa hili ni janga kwa afya ya jamii.

Pia utafiti huo ulibainisha kwamba asilimia 31  ya wazazi hawajui kutambua dalili za mtoto aliyenenepa kupita kiasi.

Aidha utafiti huo ulielezea kuwa takribani mtoto mmoja kati ya watano ambao wanaumri wa miaka 6 tayari wanauzito unaozidi kadri kwa asilimia 14%.

Katika utafiti huo kundi la watafiti kutoka Taasisi ya Usafi ya Uingereza ''London School of Hygiene and Tropical Medicine'' lilizitembelea familia 3,000 na kuwahoji iwapo watoto wao walikuwa ni wanene kupita kiasi wastani ama wembamba?

Naye Proffesa Russell Viner, wa Chuo cha Afya ya Watoto aliiambia BBC kuwa wazazi wa kisasa wanamajukumu mengi na hivyo watoto wao hutunzwa na wafanyakazi kwa asilimia, huku muda mwingi wazazi wakiwa kazini.

''Hili ni janga ambalo linatokota, madhara yake yataonekana siku za usoni katika njia ya maradhi mengi yanayohusiani na unene'' alisema Professa Viner.

Hali kadhalika naye Dkt Dame Sally Davies, alisema kwamba, ''afya ya watoto kwa sasa imehujumiwa na dhana kuwa japo mtu ni mnene jamii haitambagua kwani watu wengi duniani ni wanene''

"Nafikiri kwamba itatubidi tuwaelimishe wazazi kuhusiana na maswala ya afya ya watoto wao na pia kuwaeleza kuwa wanapaswa kufuatilia kwa karibu unene au sio wa watoto wao'' alisema daktari huyo huku akipendekeza kuwa na sheria madhubuti zinapaswa kutungwa ilikuzima matangazo ya kufana ya vyakula vyenye mafuta mengi


Anza kutangaza nasi biashara yako kwa gharama nafuu sana tujaribu sasa uamini haya tuyasemayo, piga simu namba 0758 163 818,  0672 060 006. Karibu sanaNo comments:

Post a Comment