Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 7 March 2015

HILIKI NI KIUNGO AMBACHO NI TIBA YA MAGONJWA MBALIMBALI
Hiliki ni kiungo kizuri cha kukoleza vyakula mbalimbali ambacho hutokana na mbegu zilizokauka za mmea wa hiliki.


Kiungo hiki kina viini mbalimbali ambavyo ni pamoja na protini, madini ya chokaa (calcium), phosphorus na chuma.

Aidha, hiliki pia ina dawa lishe mbalimbali mfano, quercetin, kaempferol, luteolin. Dawa lishe hizo huwezesha hiliki kuwa na harufu nzuri ya asili na uwezo wa kutibu na kutoa kinnga ya magonjwa mbalimbali.

Miongoni mwa faida za hiliki ni pamoja na kuimarisha afya ya mfumo wa kusaga na kusharabu chakula pamoja na kuchochea uzalishaji wa nyongo kwa ajili ya kuyeyusha vyakula vyenye mafuta mengi.

Pamoja na hayo pia hiliki hupunguza gesi tumboni , kiungulia sambamba na maumivu ya tumbo.

Mbali na hayo hiliki pia husaidia kutuliza kwikwi, huku ikisaida kuimarisha afya ya akili kwa kupunguza msongo wa mawazo.
Hali kadhalika hiliki pia husaidia kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na tatizo la ubaridi wa kike. 

Mandai Harbal Clinic inapenda kukufahamisha kuwa endapo unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu unaweza kufika Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na ukakutana na mtaalam wa tiba asili Dk, Abdallah Mandai ili kumaliza shida yako hiyo. Ili kufika unaweza kupiga simu namba 0758 163 818, 0672 060 006, Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment