Friday, 20 March 2015

HUU NDIO MKAKATI WA SIERRA LEONE KATIKA KUTOKOMEZA KABISA UGONJWA WA EBOLA
Katika harakati za kuangamiza kabisa janga la ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone, taifa hilo linasema kuwa
juma lijalo litawazuia karibu watu milioni mbili unusu majumbani mwao kwa siku tatu.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa Serikali ya nchi hiyo, ambapo alisema kuwa shughuli hizo zitaanzia mji mkuu Freetown na kaskazini mwa nchi hiyo, kati ya Machi 27 na 29.

Katika zoezi hilo wafanyakazi wa kimatibabu watatembelea kila nyumba ili kubaini dalili za ugonjwa huo, huku wakiwakumbusha wananchi hatari ya kushika maiti na kuwapeleka wagonjwa wa ebola kwa madaktari wa tiba ya kiasili kutokana na ugonjwa huo kutotibika hata kwa madaktari hao.

Hata hivo, hadi sasa hakuna kisa chochote cha ugonjwa huo ambacho kimeripotiwa nchini Liberia, katika kipindi cha majuma matatu yaliyopita, lakini visa vya ugonjwa huo vinaripotiwa kila juma nchini Sierra Leone na Guinea.

Unaweza kutangaza na tovuti hii ya www,dkmandai.com kwa gharama nafuu sana wasiliana nasi sasa kwa namba za simu zifuatazo  0758 163 818, 0672 060 006. Au tutumia tangazo lako kwenye email yetu ya dkmandaitz@gmail.com. Tupo tayari kutangaza na wewe sasa.

No comments:

Post a Comment