Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 24 March 2015

IKIWA LEO NI SIKU YA KIFUA KIKUU DUNIANI DK MANDAI ANAHAYA YA KUKUJUZA KATIKA SIKU HII
Ikiwa leo Marchi 24 ni siku ya Kifua Kikuu duniani Dk Abdallah Mandai anapenda kukujuza haya machache kuhusu ugonjwa huo.


Dk Mandai anasema kwamba ugonjwa wa Kifua Kikuu huathiri watu wa rika zote na hasa vijana ambao ndiyo nguvu kazi katika nchi nyingi hapa duniani.

Ugonjwa huu kitaalam unafahamika kama ‘tuberculosis’ na ni ugonjwa ambao unauwezo wa kuenea kwa njia ya hewa, huku ukienezwa na bacteria au kimelea aina ya ‘mycobacterium tuberculosis.’

Mtu anapopata maambukizi ya ugonjwa huu kwa kawaida huathirika mapafu, lakini pia huweza kushambulia viungo vingine vya mwili kama vile tezi za limfu, ubongo na mifupa.
Aidha, Dk Mandai anasema kwamba pale inapotokea mtu mwenye kifua kikuu, hajaanza tiba anapokohoa au kupiga chafya, kutema mate au makozi, hii huweza kusababisha maambukizi kwa mtu mwingine endapo atavuta hewa yenye vimelea hivyo na kisha kupata ugonjwa huo.
 
Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii zinaonesha kuwa mwaka 2013 wagonjwa wa Kifua Kikuu 65,000 waligunduliwa hapa nchini, huku  takwimu hizo zikionesha maambukizi mapya yanatokea miongoni mwa rika la vijana wenye umri kati ya miaka 25 na 44, kama ilivyo Virusi Vya Ukimwi.

Pia kwa mujibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaainisha kwamba kila mwaka wagonjwa wapatao 63, 000 hugundulika.

Dk Mandai pia anabainisha dalili za ugonjwa huu kuwa ni kukohoa kwa muda usiopungua wiki mbili na mara nyingine kukohoa damu, homa za jioni za mara kwa mara, kutokwa na jasho usiku, kukosa hamu ya kula, kupungua uzito kwa kiasi kikubwa.

Pia anashauri kwamba mgonjwa mwenye kusumbuliwa na Kifua Kikuu anashauriwa kula mlo kamili wenye ‘protein’, vitamini na ‘carbohydrate’  na vyakula vyenye protini ambavyo ni pamoja na mayai, maziwa, maharage na soya. Vyakula hivyo hujenga misuli na kuzalisha chembe za damu. Vilevile husaidia mfumo wa kinga ya mwili kupata nguvu.


Kuna njia mbalimbali za kujikinga na ugonjwa wa kifua kikuu, zipo zile ambazo hutolewa kabla mtu hajapata ugonjwa huo, ambapo chanjo ya kuulinda mwili.

Hali kadhalika Dk Mandai anasema kuwa kabla ya kuanza tiba ya kifua kikuu ni vizuri kwenda hospitali kwanza na upimwe na kuthibitisha kama ni kifua kikuu, lakini pia unaweza kutumia kitunguu swaumu kama tiba ya ugonjwa huu.

Pondaponda punje 18 za kitunguu swaumu, kisha loweka ndani ya glasi ya maji na uongeze vijiko vitatu vya mezani vya asili kisha koroga vizuri.

Baada ya hapo gawanya mchanganyiko huo katika sehemu tatu zinazolingana na unywe mara tatu kwa siku na uendelee na tiba hiyo kwa muda wa miezi miwili na wakati unaendelea na tiba hii ikiwa ukahisi maumivu kifuani na hali ya kichomi, sugua kitunguu swaumu kilichopondwa katika sehemu zote za maumivu.

Mbali na hayo Dk Abdallah Mandai ambaye ni mtaalam wa tiba asili na Mkurugenzi wa kituo cha Mandai Herbalist Clinic anapenda kutoa wito kwa Watanzania na kuwasihi kuacha kudharau matatizo yoyote ya kifua kwa sababu hakuna kifua cha kawaida, na hivyo kila anayekohoa ni vyema kufika hospitali ili kuchunguzwa zaidi na kupata ushauri wa daktari na vipimo.

Unaweza kuwasiliana na DK Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. No comments:

Post a Comment