Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Wednesday, 18 March 2015

JE, ULIKUWA UNAFAHAMU HUU UWEZO MWINGINE WA NDIZI KATIKA TIBA? PATA KUFAHAMU HAPANdizi ni tunda muhimu Afrika Mashariki na katika nchi za joto na hasa katika visiwa vya Caribbean, mmea wake huitwa mgomba.

Tunda hili ambalo lina asili ya Kusini mwa Asia huonekana na rangi nzuri na mara nyingi tumezoea kuliona shambani au maeneo ya sokoni na limeonekana kuwa na faida nyingi kiafya.
Miongoni mwa faida za tunda hili ni pamoja na kusaidia kukukinga na kupata vidonda vya tumbo kutokana na ‘compounds,’ mbalimbali zilizomo ndani ya tunda hilo.
Virutubisho hivyo ambavyo hupatikana kwenye ndizi hujenga tabaka nene kwenye kuta za tumbo ambazo husaidia tumbo kuzuia kuathirika na tindikali ijulikanayo kama ‘hydrochloric acid.’
Aidha, ndizi zina ‘enzyme’ inayojulikana kama protease inhibitor,’ ambayo huzuia bacteria wasababishao vidonda vya tumbo.

Mbali na hayo tunda hili pia linauwezo mkubwa wa kuboresha ngozi, hususani maganda yake ambayo huaminika kusaidia kuimarisha ngozi pale yanaposagwa vizuri na kuchanganywa na matunda mengine hususani parachichi.
Ambapo mchanganyiko huo kwa pamoja husaidia kulainisha ngozi na kuifanya kuonekana vizuri na yenye kung’aa.
Ndani ya ndizi kuna vitamin B6 na vitamini C, lakini vitamini B6 ndio hupatikana kwa kiwango kikubwa zaidi ndani yatunda hilo kuliko vitamini C ambayo ni kidogo.
Hali kadhalika, ndizi husaidia kuongeza idadi ya chembechembe nyeupe za damu hivyo huweza kumsaidia mtu katika kuboresha kinga mwilini.
Pia kutokana na tunda hili kuwa na sukari ijulikanayo kama glucose huweza kumsaidia mtumiaji kupata nguvu mwilini mara anapolitumia tunda hili.
Faida nyingine za ndizi ni pamoja na kuongeza nguvu mwilini, hii ni kwa sababu tunda hili huwa na sukari ijulikanayo kama‘glucose,’
Hayo ndiyo machache kuhusu tunda hili endelea kuwa karibu na tovuti hii ili kuyafahamu mengi zaidi kuhusu afya na tiba asilia kwa ujumla. Pia hakikisha unajitahidi kujenga tabia ya kupenda kula matunda mara kwa mara.

Kama ungependa kutangaza na tovuti hii yenye kutembelewa na watu wengi zaidi usipate tabu tupigie simu namba, 0758 163 818,  0672  060 006, 0652 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.
Gharama zetu ni nafuu sana Karibu 
 

No comments:

Post a Comment