Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 25 March 2015

JE, UNATATIZO LA KUTOTUNZA KUMBUKUMBU? FANYA HAYA YAFUATAYO KUONDOKANA NA TATIZO HILOTatizo la kusaha ni moja ya tatizo ambalo huwakumba watu wa rika mbalimbali hususani wale wenye umri mkubwa.


Kuna baadhi ya watu wenye tatizo hili la kusahau sana hadi kufikia hatua ya kusahau hata kula na ukimuuliza leo umekula au hujala mtu wa namna hiyo anaweza kukujibu kwamba 'sikumbuki vizuri'
 
Pia kuna baadhi ya watu wenye umri mdogo lakini wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hili na hata kupelekea wakati mwingine kushindwa kufanya vizuri katika masomo kutokana na kusahau kile kinachofundishwa darasani/ shuleni/ chuoni.

Mandai Herbal Clinic inakujuza haya yafuatayo yatakayo kusaidia kutunza kumbukumbu.

Kwanza kabisa ni matumizi ya maua ya komamanga, ambapo utahiitaji kukusanya machipukizi ya maua ya komamanga  na kuyakausha katika kivulina baadaye kuyasaga hadi yawe unga na kutunza unga huo katika chupa safi yenye  mfuniko.

Kisha utakuwa ukitumia nusu kijiko cha chai cha unga huo katika maji ya uvuguvugu mara tatu kwa muda wa mwezi mmoja.

Njia nyigine ni kutumia, rozimeri hii husaidia kutunza kumbukumbu ambapo mhusika atatakiwa kutengeneza kikombe kimoja cha chai ya majani ya rozimeri (mabichi au makavu) kisha ongeza asali kijiko kimoja cha mezani.  Koroga, kunywa , fanya zoezi hilo asubuhi na jioni kwa muda wa miezi miwili  hadi mitatu.

Pilipili Manga, chukua kijiko cha chai cha unga wa pilipili manga kisha changanya na kijiko kimoja cha chai cha asali nautmie kwa kulamba polepole kila asubuhi na jioni.
Hali kadhalika unapokula wali na maziwa mtindi kila mara huweza pia kuimarisha uwezo wako wa kutunza kumbukumbu zaidi.

Sambamba na hayo pia ni vyema kuzingatia kupata muda wa kupumzika vizuri pamoja na kula vyakula vyenye virutubisho vya kutosha na kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi yote hayo yatakusaidia pia kuongeza uwezo wako wa kutunza kumbukumbu vizuri. 

Pia unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata ufumbuzi wa magonjwa yako yanayokusumbua. Wasiliana sasa na Dk Abdallaha Mandai kwa simu zifuatazo,0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment