Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 28 March 2015

JERRY SLAA ATEMBELEA MANDAI HERBAL CLINIC NA MANDAI ENTERTAINMENT NA KUTOA PONGEZI KWA DK MANDAI


Meya wa Ilala Jerry Slaa amempongeza Dk Abdallah Mandai kwa kuendelea kutoa huduma za matibabu bora kwa kutumia mimea na matunda.

Hayo aliyasema alipotembelea Mandai Herbal Clinic na Mandai Entertainment leo Jumamosi Marchi 28, na kusema kwamba, Dk Mandai anastahili pongeze kwa juhudi zake za kuhudumia jamii ya Watanzania na wakazi wa Ukonga kwa ujumla. 

Hali kadhalika Slaa amesema kuwa, tiba asili ni nzuri na kimsingi hata tiba za kisasa zinauasilia ndani yake lakini huenda kwa ajili ya kukosa mimea (miti) ndio maana wataalam wa tiba hizo za kisasa hulazimika kutengeneza dawa zao kwa marighafi ambazo si asilia(artificial.) 

Mkurugenzi Mkuu wa Mandai Herbal Clinic na Mandai Entertainment, Dk Abdallah Mandai (kulia) akizungumza na Meya  wa Ilala Jerry Slaa katika studio za Mandai Entertainment.
Pamoja na hayo, Slaa amewataka wananchi hususani vijana kupenda kufanya kazi kwa bidii na kuacha dhana ya kuaamini kwamba serikali itawafanyia kila kitu.


Kuna mengi ambayo alizungumza Jerry Slaa ikiwa ni pamoja na muziki, wasanii na masuala ya siasa ambayo yote unaweza kuyapata kupitia www.mandaientertainment.com siku chache zijazo.

Unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 44.

No comments:

Post a Comment