Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 5 March 2015

KULA VYAKULA BORA KUTAKUSAIDIA KUWA NA AFYA BORA NA FURAHA
Tunapozungumzia chakula bora mara zote humaanisha ni kile chakula ambacho ndani yake huweza kumpatia mlaji virutubisho vyote muhimu vinavyohitajika ndani ya mwili wa mwanadamu kwa ajili ya siha nzuri ya mwili.

Unapokula vyakula vilivyo bora katika maisha yako tambua itakusadia sana kukufanya kunjenga mwili wako vizuri sambamba na kukufanya kuishi kwa kuwa mtu mwenye amnai na furaha kila siku.

Mandai Herbal Clinic inapenda kukupatia haya machache juu ya vyakula bora ili wewe msomaji wa tovuti yetu hii uweze kuzingatia kufuatilia kula vyakula hivyo ili kuwa na afya bora zaidi.

Miongoni mwa vyakula hivyo bora ni pamoja na matunda yaliyo freshi, mboga freshi, kuku wa kienyeji na mayai yake pamoja na maji glass 8 kwa siku.


Vingine ni maziwa, asali mbichi kiasi cha kijiko kimoja cha chai kila siku, pamoja na juisi fresh ya matunda.

Hiyo tunaweza sema ni vyakula vinavyoweza kukufaa kwa ujenzi wa afya yako, lakini pia vyakula ambavyo huweza kuhatarisha afya ni pamoja na matumizi ya sukari nyingi na chumvi nyingi, ulaji wa nyama nyekundu pamoja na kutumia nafaka zilizokobolewa kama mkate mweupe nk.

Vingine ambavyo ni hatari kwa afya yako ni matumizi ya pombe, sigara  hali kadhalika na unywaji wa vinywaji baridi.


Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa sugu unaweza kukutana na Dk Abdallah Mandai sasa na ukapata ufumbuzi wa matatizo yako, kliniki ipo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na inaitwa Mandai Herbal Clinic au unaweza kupiga simu namba  0758 163 818, 0672 060 006, Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment