Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 17 March 2015

MAHINDI PALE YANAPOTUMIKA KAMA TIBAMahindi ni zao ambalo hulimwa sana sehemu mbalimbali hapa nchini na zao hili huhesabika kama zao la chakula.


Mtaalam wa tiba asili Dk, Abdallah Mandai anasema kwamba majani na mizizi yam mea huo husaidia kutibu figo pamoja na kibofu cha mkojo.

Aidha, mtaalam huyo, anabainisha kuwa ndevu za mahindi ni dawa ya maumivu yanayoweza kumpata mtu wakati wa kukojoa pia ndevu hizo husaidia uvimbe wa miguu.

Pamoja na hayo, mmea huo huweza kuwasaidia watu wenye shida katika kukojoa hasa kwa wanaume wazee pamoja na watoto wenye shida ya kukojoa kitandani.

Dk, Mandai anaeleza kuwa mizizi na majani ya mahindi inapowekwa katika maji ya moto na kuchunjwa ndio huweza kuwa tiba.

Mbali na hayo, anaeleza kuwa pia mgonjwa anapochukuwa ndevu za mahindi za kutosha na kuchemsha katika maji kisha kunywa kwa siku tano huwa ni tiba au kinga ya magonjwa tajwa hapo juu.

Mandai Herbal Clinic inaendelea kukukumbusha kwamba endapo unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu unaweza kufika kituoni kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata suluhisho la matatizo yako. Pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.    

No comments:

Post a Comment