Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 26 March 2015

MAJARIBIO YA CHANJO YA EBOLA YAFANYIKA NCHINI GUINEASerikali ya Guinea na Shirika la Afya Duniani, WHO, zimezindua majaribio ya kwanza kabisa ya chanjo ya Ebola wiki hii katika jamii iliyoathiriwa ya Basse-Guinée, ambayo ni moja ya maeneo ambako visa vya Ebola ni vingi zaidi nchini humo.


Jaribio hilo la dawa ya chanjo aina ya VSV-EBOV iliyoundwa na Shirika la Afya ya Umma, Canada, limepokewa vyema na jamii katika kijiji kimoja katika kata ya Coyah, ambako timu ya kufanyia chanjo hiyo jaribio iliwasili mnamo Machi 23 mwaka huu wa 2015.

Kwa upande wa mwakilishi wa WHO nchini Guinea, Jean-Marie Dangou, amesema operesheni hiyo ya aina yake inatoa matumaini kwa wote Guinea na dunia nzima kwamba huenda kukawa na chombo stahiki cha afya ya umma dhidi ya Ebola hivi karibuni, iwapo dawa hiyo ya chanjo itadhihirika kuwa salama na yenye kufanya kazi ipasavyo.

Hata hivyo, imeelezwa kwamba kwa wakati huu, chanjo itawahusisha watu wazima pekee, ambao wamo hatarini zaidi kuambukizwa, ingawa waja wazito hawatafanyiwa jaribio la chanjo.

No comments:

Post a Comment