Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 7 March 2015

MAUA YA MABOGA NI TIBA YA UGONJWA WA MTOTO WA JICHOUgonjwa wa mtoto wa jicho hutokea pale ambapo mtu anapokuwa amejeruhiwa katika chembe hai zinazohusika na utengenezaji wa lensi ya jicho.

Jeraha hilo huweza kuchangiwa na matumizi ya muda mrefu ya jicho husika na hivyo  kusababisha hali hiyo mara nyingi kuwakuta watu wenye umri mkubwa zaidi.

Aidha, sababu nyingine za tatizo hili huweza kuwa pengine ni majeraha ya moja kwa moja kwenye jicho. Mfano ajali.

Pia maradhi ya kisukari husababisha tatizo hili hii ni kutokana na maradhi hayo kuhusiana sana macho.

Wengine huweza kupata maradhi haya kutokana na sababu za kurithi hii huchangiwa na hitilafu katika utengenezwaji wa chembe hai zinazohusika na kuiunda lensi ya jicho.

Kwa ujumla maradhi haya hutokea pale ambapo chembe hai zinazotengeneza lensi ya jicho kujeruhiwa na hivyo kuunda lensi yenye mapungufu na ambayo haina uwezo wa kupokea mwanga wa taswira kama vile ulivyoingia kwenye jicho kwa kupitia sehemu ya mbele.

Kitu kikubwa kinachotokea kwenye maradhi haya ni usambazaji mbovu wa mwanga huu wa taswira unapofika kwenye lensi. Hii husababisha na kutokuwa na unyoofu wa  mazingira katika ukuta wa lensi uliotokana na kujeruhiwa kwa chembe hai zake zinazoundwa.

Hata hivyo ni vyema ikafahamika kuwa kadri binadamu anavyoendelea kuongezeka kiumri lensi ya jicho/macho hupunguza uwezo wake wa kufanya kazi, hii ni kutokana na kushindwa kwa lensi kutanuka na kusinyaa vizuri ili kufanikiwa kuelekeza mwanga ule wa taswira kuelekea kwenye retina.

Pia mabadiliko hayo ya kiumri husababisha chembe hai zinazotengeneza lensi kushindwa kufanya kazi vizuri hivyo kusababisha tishu zinazoundwa na chembe hai hizi kujazana au kuvunjika kisha kukaa pamoja na kutengeneza ukungu unaoota juu ya lensi.

Mtu mwenye tatizo hili huweza kupata shida hii kwenye jicho moja tu, lakini kwa waliowengi hupata kwenye macho mawili yote.

Mtaalam wa tiba asili kutoka Mandai Herbal Clinic, Dkt Abdallah Mandai anasema kuwa, tatizo la mtoto wa jicho huweza kutibika licha ya kuwa tiba yake huchukuwa muda mrefu na hivyo kumtaka mgonjwa kuwa mvumilivu.

Tiba za tatizo hili zipo nyingi, lakini hapa Dkt, Mandai anakufahamisha hii ya maboga tu na ikiwa unapenda kuzifahamu nyinginezo basi utaweza kufika Mandai Herbal Clinic ili kujua zaidi.

Dkt, Mandai anasema kuwa maua ya maboga ndiyo hutumika katika tiba hii, ambapo mhusika atachukuwa maua ya maboga na kutengeneza juisi yake kisha unapaka juisi hiyo kwenye kope za macho asubuhi na jionii kwa muda wa mwezi mmoja.

 Mandai Harbal Clinic inapenda kukufahamisha kuwa endapo unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu unaweza kufika Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na ukakutana na mtaalam wa tiba asili Dk, Abdallah Mandai ili kumaliza shida yako hiyo. Ili kufika unaweza kupiga simu namba 0758 163 818, 0672 060 006, Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment