Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 30 March 2015

MLO KAMILI HUCHANGIA MAMA MJAMZITO KUJIFUNGUA MTOTO MWENYE AFYA
Mama mjamzito hupaswa kula mlo kamili muda wote wa kipindi cha ujauzito kwa lengo la kusaidia ukuaji wa mtoto tumboni.


Mama mjamzito anapaswa kula mlo wenye vitamini na madini yote muhimu ambayo ni muhimu sana kwa ukuaji wa mtoto tumboni na uimarishaji wa afya ya mama na kumuepusha na matatizo mengine ya kiafya yanayoambatana pamoja na ujauzito.

Pia kipindi cha ujauzito, mlo unaoshauriwa kuliwa zaidi ni ule wenye madini ya ‘calcium’ ‘foliki asidi’, protini na vitamini B12. Vyakula vyenye kiwango kikubwa cha ‘calcium’ ni pamoja na mtindi, jibini, maziwa yasiyo na mafuta  pamoja na maharage, n.k.

Vyakula vyenye kiwango kikubwa cha madini ya ‘foliki asidi’ ni pamoja na karanga, siagi ya karanga (peanut butter), maharage makavu, mahindi na mboga za majani pia.

Aidha, katika kipindi chote cha ujauzito, mama anatakiwa kuhakikisha anazingatia suala la kula lishe bora ili kuhakisha ubongo wa mtoto, mifupa na viungo vingine muhimu vinakuwa vizuri. 

Pamoja na hayo pia ni vizuri mama mjamzito kula kidogo kidogo kila mara kwa ratiba maalum  pamoja na kunywa maji mengi, angalau glasi nane kwa siku.

Mbali na hayo, mama mjamzito pia anashauriwa kula mlo kamili yaani (balanced diet), huku akiepuka matumizi ya sigara, unywaji pombe na vinywaji vyenye ‘caffeine’, kama vile chai, soda, n.k.

Ikiwa unapenda kutangaza biashara yako kupitia tovuti yetu hii kwa gharama nafuu sana basi wasiliana nasi kwa simu namba , 0758 163 818, 0672 060 006, pia like ukurasa wetu wa facebook uitwao Mandai Herbalist Clinic- mhc na utafikiwa na taarifa za tiba kila siku

No comments:

Post a Comment