Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Tuesday, 17 March 2015

MUUGUZI ATEKWA DAR
Muuguzi wa Hospitali ya Mwananyamala, Pili Amiri ametekwa na watu wasiojulikana na kisha kutoa masharti  ya kupewa kiasi cha shilingi milioni 5 ili wamuachie huru.


Muuguzi huyo mwenye umri wa miaka 26, alitekwa akiwa nyumbani kwake Mwananyamala,  Komakoma saa tano asubuhi, Alhamisi ya wiki iliyopita na kuingizwa katika gari linalodaiwa kuwa ni la watekaji hao.

Akizungumzia tukio hilo mjomba wa Pili, Rahim Kangile alisema watekaji hao baada ya kumteka walipiga simu kwa kutumia namba ya Pili wakidai kutumiwa kiasi hicho cha fedha.

“Waliposema wanataka sh milioni 3 ili wamuachie , tuliwatumia lakini hawakufanya hivyo hadi jana wakasema tuwatumie tena shilingi milioni 2 tumetuma leo (jana) lakini mpaka sasa hakuna chochote tulichofanikiwa” alisema.

Kangile aliendelea kusema kwamba, watekaji hao walitoa vitisho kuwa endapo malipo hayo hayatafanyika basi watafanya lolote baya kwa muuguzi huyo.

“Tulipoona wanatoa vitisho tuliwatumia hizo hela lakini hawajafanya chochote la kuonesha watamua watamuachia  Pili” alisema.

Aidha, alisema watekaji hao walitaka fedha zitumwe katika akaunti ya NMB ya Pili, jambo ambalo lilitekelezwa na baadaye ikabainika kuwa miamala kadhaa imefanywa kupitia mtandao wa ATM kutoka kwenye akaunti ya muuguzi huyo.

Akizungumzia endapo Pili aliwahi kuwa na maadui, Kangile alisema hawana chembe ya shaka kama muuguzi huyo alikuwa na ugomvi na watu hadi kufikia hatua ya kumteka.

Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk Sosphiniasis Ngonyani alisema Pili hakutekwa akiwa mazingira ya hospitali, bali akiwa nyumbani kwake na kueleza kuwa wanafamilia wametakiwa kutoa kiwango hicho cha fedha ili aachiwe huru.

“Ni kweli huyu muuguzi wetu ametekwa tangu Alhamisi iliyopita, tumezipata taarifa kutoka kwa ndugu zake, baada ya kutokuonekana nyumbani kwa siku kadhaa” alisema.

Dk Ngonyani alisema polisi wameshapata taarifa za tukio hilo na wanaendelea kufanya kazi yao ili kupata taarifa za ndani zaidi.

Kwa upande wa Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, Camillius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mpaka sasa hawana uhakika kama ni utekaji au nesi huyo ametoweka katika mazingira ya kutatanisha.

SOURCE: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment