Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 3 March 2015

MWALIMU ALIYEKUWA AKIISHI NA KINYESI AFIKISHWA HOSPITALI YA MUHIMBILI KWA MATIBABU ZAIDI
Mwalimu wa shule ya sekondari Kibasila Dar es Salaam Gaudensia  Albert, aliyekuwa akihifadhi kinyesi ndani kwake amefikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.


Akizungumzia suala hilo Mwalimu Mkuu wa Msaidizi wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Malimu Kyando alisema hapo awali baada ya kugundulika kuwepo kwa tukio hilo  Mwalimu Gaudensia alipelekwa hospitali ya Temeke ili kuangalia afya yake.

Mwalimu huyo alisema baada ya kufika hospitalini hapo walipewa taarifa na daktari kuwa alikuwa na tatizo la akili ambapo alipata uhamisho wa kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

“Baada ya kupata taarifa ile kiukweli tulishtushwa kulingana na taarifa iliyotufikia”alisema

Aliongeza kuwa baada ya kufikishwa hospitali ya Muhimbili wataalam walisema kutokana na hali yake walimpatia dawa ambazo hadi sasa anatumia pamoja na kupatiwa ushauri.

Mwalimu huyo ambaye kwa sasa anaishi kwa ndugu zake bado anatumia dawa, huku akipatiwa ushauri wa kitaalam ili kumuweka sawa kiakili.

“Tangu alipoanza matibabu hali yake inaendelea vizuri na endapo akipona kabisa atarejea kwaajili ya masomo yake kama ilivyokawaida” alisema.

Hata hivyo mwalimu huyo mkuu msaidizi alisema kuwa licha ya kukutwa na matatizo hayo kwenye nyumba aliyokuwa akiishi, lakini mwalimu huyo alikuwa akifundisha vizuri shuleni hapo.

Huku akiongeza kusema kuwa “sisi bado tunamhitaji kutokana na uhaba wa wawalimu wa mchepuo wa sayansi”

Itakumbukwa kwamba Mwalimu Gudensia ni mwalimu wa masomo ya Baiolojia na Kemia na ilibainika alikuwa akiishi na kinyesi maeneo ya Yombo kisiwani katika nyumba ya Ruben Shayo ambapo ilidaiwa kuwa mwalimu huyo aliishi na kinyesi ndani kwake kwa muda wa miaka miwili

SORCE: JAMBO LEO

No comments:

Post a Comment