Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 4 March 2015

NCHI KUKUBWA NA UKAME NA HUENDA MAGONJWA YA MLIPUKO YATATOKEADk.Agnes Kijazi (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam.
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa taarifa ya mwelekeo wa mvua za masika katika kipindi cha mwezi Machi hadi Mei.


Taarifa hiyo imetolewa hapo jana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo amesema hali ya mvua haitarajiwi kuwa ya kuridhisha katika maeneo mengi hapa nchi.

Kufuatia hali hiyo Dk Kijazi alisema maeneo mengi yatakumbwa na ukame.Aidha, huku akiitaja mikoa inayotarajiwa kupata mvua za wastani mpaka chini ya wastani kuwa ni Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Unguja na Pemba, Morogoro, Kilimanjaro, Arusha na Simiyu.

Mikoa mingine ni Singida, Dodoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Kigoma, Shinyanga na Manyara ambayo pia inatarajiwa kupata kiasi kidogo cha mvua.

Hata hivyo, Dk Kijazi alisema Kanda ya Ziwa yaani mikoa ya Mwanza, Geita, Mara na Kagera inatarajiwa kupata mvua za wastani mpaka juu ya wastani.

 “Mikoa ya kanda ya Ziwa Victoria inaweza kupata mvua za wastani mpaka juu ya wastani, hivyo mamlaka husika zinapaswa kujiandaa kwa hali yoyote inayoweza kujitokeza,” alisema Dk Kijazi.

Mbali na hayo aliongeza kusema kuwa “wasimamizi wa maeneo ya utalii wachukue hatua ya kuzuia uharibifu wa miundombinu ya barabara na madaraja katika mbuga zilizo karibu na maeneo ya Ziwa Victoria.”

Sambamba na hayo naye Mtaalam wa Afya ya Jamii kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jubilate Benard, alisema kuna hatari ya kutokea kwa magonjwa ya mlipuko kwenye maeneo yatakayopata mvua nyingi.

Hali kadhalika kwa upande wa sekta ya kilimo Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula, Karim Mtambo aliwataka wakulima wanaoishi katika maeneo yatakayopata mvua za chini ya wastani kulima mazao yanayokomaa haraka na kustahamili ukame.

Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa sugu unaweza kukutana na Dk Abdallah Mandai sasa na ukapata ufumbuzi wa matatizo yako, kliniki ipo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na inaitwa Mandai Herbal Clinic au unaweza kupiga simu namba  0758 163 818, 0672 060 006, Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment