Wednesday, 25 March 2015

NIMEKUWEKEA HAPA NJIA TATU ZINAZOWEZA KUPONYA VIDONDA KWA HARAKA ZIPO PIA ZABIBUKatika maisha yetu ya kila siku huwa inafika wakati tunapata majeraha kutokana na sababu mbalimbali inaweza kuwa za kikazi au shughuli tu za nyumbani na hivyo kutusababishia vidonda ambavyo mara nyingine huwa ni ngumu kupona kwa haraka.


Lakini leo hii Mandai Herbal Clinic inapenda kushare na wewe msomaji wetu wa tovuti hii hizi njia tatu zinzoweza kuponya vidonda kwa haraka.

Hata hivyo, kabla ya kukujuza njia hizo kwanza ni vyema ikatambulika kwamba tiba hii tutakayokujuza itategemeana na ukubwa wa kidonda, muda gani mgonjwa amekuwa na kidonda hicho, chanzo cha kidonda, dawa za awali ambazo zilitumika kutibu kidonda hicho.

Miongoni mwa njia hizo za asili ambazo zitaweza kuwa tiba kwa vidonda ni hii ya kutumia zabibu, tiba hii kinachopaswa kufanyika ni kuchukuwa zabibu zilizokaushwa, ponda ponda ili kutengeneza aina ya ujiuji kisha chukuwa kitambaa safi kinachotosha kuenea sehemu yote ya kidonda. Paka ujiuji wa zabibu kwenye kitambaa hicho halafu weka kitambaa kingine kinacholingana juu yake, bandika kwenye kidonda kisha funga na kitambaa kingine.

Zabibu hiyo inauwezo wa kunyonya sumu kutoka kwenye kidonda. Rudia utaratibu huo mara nne kwa siku na baada ya siku mbili mara mbili kwa siku.

Utomvu wa papai pia ni tiba ya kidonda, ambapo inatakiwa kuchanganywa utomvu wa papai na mafuta ya ng’ombe kisha paka kwenye kidonda asubuhi na jioni. Tiba hii inasaidia hata wenye vidonda ndugu.

Kitunguu maji, pondaponda kitunguu maji kisha maji yake paka kwenye kidonda kilichosafishwa. Fanya hivyo asubuhi na jioni hadi pale kidonda kitakapo pona
  
Unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. No comments:

Post a Comment