
Hivi sasa magonjwa ya ysiyoambukiza hususani ya moyo yamekuwa yakishika kasi na kusumbua watu wengi kwa ujumla.
Kwa mujibu wa Taasisi ya Magonjwa ya Moyo nchini
India, watu milioni 2.4 hufariki dunia kila mwaka kutokana na magonjwa ya moyo,
huku sehemu kubwa yakichakiwa na mitindo ya kimaisha ambayo ni pamoja na kuishi
na sonono yaani stress, kutokula kwa kuzingatia taratibu za afya pamoja na
kukoosa usingizi kwa muda mrefu.
Hata hivyo kuna njia ambazo huweza kumsaidia mtu
kuepukana na magonjwa ya moyo, hii ikiwa ni pamoja na namna ya mpangilio wa
vyakula sambamba na ufanyaji wa mazoezi.
Unaweza kuepuka magonjwa ya moyo kwa kupendelea kula
matunda, mboga za majani pamoja na vyakula vya nafaka ambavyo husaidia kuondoa
hatari ya kupata magonjwa ya moyo.
Kuepuka matumizi ya sigara na tumbaku, ambayo yote
huweza kuchangia mhusika kuwa katika hatari ya kupata magonjwa ya moyo. Hivyo
endapo umekuwa ni mtumiaji wa sigara au tumbaku ni vyema ukafanya maamuzi ya
kuacha mara moja ili kujiondoa katika hatari ya kupata magonjwa haya ya moyo.
Epuka kuwa na uzito kupita kiasi, hali hii huweza
kuchangia mwili kulundikana na mfuta hatari yaani cholesterol, ambayo huwa ni
hatari kwa afya ya moyo, hivyo ni vizuri ukajenga mazoea ya kufanya mazoezi ya
mwili mara kwa mara ili kuepuka kuwa na uzito uliokithuri.
Punguza matumizi ya chumvi kupita kiasi, ulaji wa
chumvi kupita kiasi huchangia msukumo wa damu kuwa juu zaidi ambayo ni moja ya
sababu inayoweza kuchangia mhusika kuanza kukubwa na tatizo la shinikizo la
damu. Pia epuka vyakula ambavyo vimesindikwa kwa chumvi nyingi.
Jitahidi kulala kwa muda wa kutosha angalau masaa 7
hadi 8 kwa siku, kukosa usingizi huweza kusababisha mtu kukosa furaha na kuwa
mchangamfu na hata shambulio la moyo, kulala usingizi mzuri hutengeneza mtu
kuwa na mchangamfu na uwezo mzuri wa kupambanua mambo.
Jambo la muhimu pia ni kuepuka msongo wa mawazo au kukabiliana
na msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo (stress) huweza kusababisha shambulio la
moyo (heart attack) na mara nyingine hata kifo. Kufanya mazoezi ni moja ya njia
inayoweza kukusaidia kupunguza msongo wa mawazo.
Pamoja na hayo yote lakini kumbuka kwamba ni muhimu
sana kujenga tabia ya kufanya uchunguzi wa afya yako mara kawa mara kwa
kuangalia msukumo wako wa damu kama upo sawa, na kuhakikisha hauna kiwango cha
sumu mwilini pamoja na kuepukana na mgonjwa kama kisukari.
Je, unasumbuliwa na magonjwa sugu? Kama jibu ni ndio
basi hakikisha unafika Mandai Herbal Clinic iliyopo Ukongo, Mongolandege jijini
Dar es Salaam ambapo utapata nafasi ya kukutana na mtaalam wa tiba asili, Dk
Abdallah Mandai na kupatiwa dawa zisizo na kemikali zitokanazo na mimea
mbalimbali na matunda. Pia unaweza kumpigia simu Dk Mandai kwa namba zifuatazo 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua
pepe, dkmandaitz@gmail.com.
No comments:
Post a Comment