Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Saturday, 28 March 2015

PENGINE HII IKAWA NI ZAIDI YA SAYANSI BINADAMU SASA KUPANDIKIZWA MOYO!!
Kweli kuishi kwingi ni kuona mengi hivi katika maisha yako uliwahi kufikiri ipo siku wanasayansi watafikia hatua ya upandikizaji wa moyo kutoka kwa binadamu mmoja kwenda kwa mwingine?

Sasa kutana na hii ya Madaktari wa upasuaji huko Cambridgeshire  wao wamefanya upandikizaji wa kwanza wa moyo barani Ulaya kwa kutumia moyo mwengine uliosimama kufanya kazi.

Taarifa zinasema kwamba katika upasuaji huo, moyo huo ulitoka kwa mtu ambaye mapafu yake na moyo wake ulikuwa haufanyi kazi.

Ili kukamilika kwa zoezi hilo la upandikizaji huhitajika mioyo ya watu waliokufa, lakini ambao mioyo yao bado inafanya kazi. Huku Hospitali ya Papworth ikisema kuwa mbinu hiyo huenda ikaongeza idadi ya mioyo inayopatikana kwa asilimia 25.

Miongoni mwa vifaa vinavyotumika kukamirisha zoezi hilo la upandikizaji wa mioyo

Inaelezwa kuwa, mgonjwa aliyewekwa moyo mpya kwa jina Huseyin Ulucan, mwenye umri wa miaka 60, kutoka London, alikabiliwa na shinikizo la moyo mwaka 2008.

Alisema kabla ya upasuaji, sikuweza kutembea na nilichoka sana, kwa hakika sikuwa na maisha mazuri. Lakini sasa anasema kuwa amefurahishwa na kuimarika kwa afya yake tangu afanyiwe upandikizaji huo.

“Kwa sasa najisikia mwenye nguvu kila siku na nimetembea hadi haospitalini asubuhi hii bila tatizo” alisema Huseyin Ulucan

Hata hivyo, taarifa zinasema kuwa kumekuwa na visa 171 vya upandikizaji wa mioyo katika kipindi cha miaka 12 iliopita nchini Uingereza.

Lakini mahitaji yanashinda mioyo iliopo, hivyo basi wagonjwa wengine hungoja kwa miaka mitatu kupata kiungo kinachowafaa. Huku wengi wa wagonjwa hao hufariki kabla ya kiungo kupatikana.

No comments:

Post a Comment