Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Saturday, 28 March 2015

RUBANI WA NDEGE YA UJERUMANI ILIYOANGUKA NA KUWAUA ABIRIA 150 ALIKUWA NA UGONJWA WA AKILI
Mara nyingi hapa nchini mtu unapopata ajira sehemu waajiri wengi hujikita zaidi kuhakiki vyetu na wasifu wa mhusika (mwajiriwa) huku wakisahau kabisa kuangalia masuala ya afya ya mhusika.


Sasa kutokana na kutotilia maanani suala la kuhakiki afya za waajiriwa kabla ya kuwaajiri huko nchini Ujerumani taarifa zinasema kwamba, viongozi wa mashtaka nchini humo wamepata ushahidi unaosema kwamba rubani wa ndege ya Ujerumani ilioanguka katika milima ya ALPS na kuwaua abiria 150 alikuwa amemficha mwajiri wake kuhusu ugonjwa anaougua wa akili.

Maafisa hao walisema kwamba walipata kijikaratasi cha ugonjwa kilichokuwa kimekatwa ambacho kilimtaka rubani huyo kupumzika siku ya kuanguka kwa ndege hiyo.

Hata hivyo, kuhusu tukio hilo vyombo vya habari nchini Ujerumani vimeripoti kwamba faili ya rubani Andreas Lubitz mwenye umri wa miaka 27 katika shirika la anga za juu imeonyesha kuwa Andreas alikuwa na matatizo ya akili na alitakiwa kufanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara.

Rubani Andreas Lubitz


Pamoja na hayo, ripoti nyengine ambazo hazijathibitishwa zimesema kuwa alilazimika kuchukua likizo ya miezi sita kutoka kwa mafunzo ya urubani kutokana na shinikizo la akili.

Je ni mara ngapi umeenda kutafuta kazi ukakutana na hii ishu ya kuleta taarifa zako za kiafya? Unaweza kushare nasi pia katika ukurasa wetu wa facebook uitwao Mandai Herbalist Clinic -mhc

No comments:

Post a Comment