Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 10 March 2015

TAMBUA UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO (1)
Miongoni mwa magonjwa yanayoshika kasi na kuwasumbua watu wengi ni vidonda vya tumba ambavyo kwa kiasi kikubwa hutokana na mifumo mibaya ya maisha ya mwanadamu na kutozingatia aina ya vyakula sahihi kwa ajili ya kulinda afya.


Ugonjwa huu huibuka mara baada ya kutokea vidonda kwenye kuta za utumbo wa mwanadamu ambavyo hutokana na kuzidi kwa kiwango cha tindikali yenye kazi ya kuyeyusha chakula kiingiacho mwilini.

Mgonjwa anapokosa tiba ya mapema tatizo huweza kuwa kubwa zaidi hadi kufikia kwenye mishipa ya damu hivyo halikuwa mbaya zaidi.

Aidha, yapo mambo mengi yanayochangia uwepo wa tatizo hili ikiwa ni pamoja na msongo wa mawazo, aina ya vyakula, mfumo wa maisha.

Hata hivyo wataalam wa masuala ya afya wanaeleza kuwa chanzo kikubwa cha tatizo hili ni bacteria anayefahamika kwa jina la ‘Helicobacteria Pylori’

Kwa kawaida tumbo la mwanadamu huwa na tabia ya kujikinga na matatizo mbalimbali ya kiafya likiwemo hili la vidonda vya tumbo.

Tumbo hujikinga na tatizo hili kwa kuzalisha ute ute ambao hufanya kazi kama kinga ya kuzuia tindikali  aina ya haidrokloriki na kimeng’enyo cha aina ya pepsin kutoleta madhara mwilini. Ikiwa uzalishaji huu hautafanikiwa ndipo vidonda vya tumbo hutokea.

Lakini sababu ya msingi kwa tatizo hili hutokea  kwa sababu ya bacteria hao wa H. Pyori, ambao wana uwezo wa kuishi kwenye ukuta wa tumbo wakiwa chini ya ute unaofanya kazi kama kinga dhidi ya athari za tindikali .

Inapotokea udhaifu katika uzalishaji wa ute unaotumika kujikinga na madhara ya tindikali wakati wa kusaga chakula tumboni.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa matumizi ya kahawa kwa wingi husababisha uzalishaji wa tindikali kwa kiasi kikubwa.


Kwa  leo tuishie hapo, lakini endelea kuwa karibu na tovuti hii maana tutakuletea dalili za ugonjwa huu wa vidonda vya tumbo. 


Unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic ili upate suluhisho la magonjwa mengine yakiwemo yale sugu kwa kutumia tiba asili za mimea na matunda, kituo chetu kipo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.   

No comments:

Post a Comment