Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 25 March 2015

TATIZO LA MTOTO KUKOSA CHOOWatoto wadogo hususani wale ambao bado wananyonya na wale ambao ndio wameanza kula vyakula vingine zaidi ya maziwa, mara nyingi hupatwa na tatizo hili la kuwa na choo kigumu na hata kukosa choo kabisa.


Hali hiyo kitaalam huitwa ‘constipation’ mara nyingi watoto wanaonyonya maziwa ya mama huwa hawasumbuliwa sana na tatizo hilo, lakini tatizo hilo huanza kujitokeza pale wanapoanza kulishwa vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama.

Mzazi unashauriwa kumuona daktari pindi unapogundua mtoto wako anasumbuliwa na tatizo hili, lakini pia unashauriwa kujaribu njia zifuatazo:

Kwanza hakikisha unampatia mtoto maji safi na salama ya kutosha na utakuwa ukipunguza au kuongeza kiasi cha maji kulingana na hali ya mtoto inavyoendelea. Hali kadhalika unaweza kumpatia mtoto juisi za matunda pia .

Pia ni vyema kujitahidi kumpa mtoto vyakula vyenye nyuzi nyuzi endapo mtoto atakuwa ameshaanza kula vyakula vigumu.

Mbali na hayo pia unaweza kumpaka  mwanao mafuta kidogo sehemu inayotoka choo kikubwa ili kurahisisha utokaji wa kinyesi. Hakikisha mafuta unayotumia si yale yenye madini (mineral oil.)

Hata hivyo kuna baadhi ya watoto wanakosa choo au kuwa na choo kigumu kutokana na kutumia maziwa ya ng’ombe. Iwapo umetumia dawa na umefuata maelekezo ya kuondoa ukosefu wa choo na hukufanikiwa. Jaribu kukatisha kumpa mtoto maziwa ya ng’ombe kwa siku mbili au tatu, baada ya siku hizo iwapo bado hajaacha choo bado endelea kumpa maziwa hayo, na pengine tatizo hilo halisababishwi na maziwa ya ng’ombe. 

Unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment