Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Sunday, 29 March 2015

TAZAMA PICHA 20 MUHIMU ZA MEYA WA ILALA JERRY SLAA ALIPOTEMBELEA MANDAI HERBAL CLINIC NA MANDAI ENTERTAINMENT

Kwanza kabisa timu nzima ya Mandai Herbal Clinic na Mandai Entertainment tukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dk Abdallah Mandai tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Meya wa Ilala Jerry Slaa kwa kutembelea ofisi zetu na kuona kile tunachokifanya hii inaonesha ni kiasi gani Meya huyu yupo pamoja nasi, lakini pia yupo pamoja na wananchi wote wa Ilala. Asante sana Jerry Slaa

Kutoka kushoto ni Dk Mandai akimueleza jambo Meya Jerry Slaa kuhusu utanuzi wa kliniki ya Mandai Herbal Clinic na namna itakavyokuwa mara baada ya kukamilika

Mara baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa jengo la Kliniki moja kwa moja Meya Jerry Slaa alipata fursa ya kuzungumza na madereva bodaboda ambao hutoa huduma karibu kabisa na kliniki ya Dk Mandai

Dk Mandai akiwaelezea jambo madereva bodaboda na kuwatambulisha pia kwa  Meya Jerry Slaa


Madereva bodaboda wanatoa huduma karibu na Mandai Herbal Clinic wakimsikiliza Meya Jerry Slaa moja ya vitu alivyowaahidi ni kuwarahisishia mazingira yao ya kazi ikiwa ni pamoja na miundombinu (daraja)

Jerry Slaa akisisitiza kitu kwa madereva bodaboda hao
Usafiri wa Meya Jerry Slaa


Baada ya kukagua Mandai Herbal Clinic na kuzungumza na madereva bodaboda Jerry Slaa alikwenda pia kutembelea studio za Mandai Entertainment zilizopo karibu pia na Mandai Herbal Clinic
Safari ya kuelekea Mandai Entertainment ikaanza


Meya Jerry Slaa akishuka kwenye gari na kuingia Mandai Entertainment

Akipata maelekezo kidogo mapokezi ya Mandai Entertainment kabla ya kusaini katika kitabu cha wageni

Meya Jerry Slaa akisaini katika kitabu cha wageni baada ya kufika Mandai Entertainment (Mandai studio)


Hapa Meya Jerry Slaa akiwa katika ofisi ya Mandai Entertainment akipokea maelekezo kutoka kwa Dk Mandai (ambaye hayupo pichani) akimueleza kuhusiana na shughuli za Mandai Entertainment

Hapa Dk Mandai (kulia) akiwa na Meya Jerry Slaa katika moja ya sehemu maalum za studio za Mandai Entertainment kwa ajili ya kurekodia vipindi mbalimbali vya luninga ambapo pia Jerry alipata nafasi ya kufanya mahojiano na mtangazaji wa Mandai Entertainment juu ya masuala mbalimbali. Mahojiano hayo utaweza kuyaona kupitia Channel Ten Jumatano saa 11:30 jioni


Hapa mtangazaji kutoka Mandai Entertainment Idrissa Anelco akifanya mahojiano na Meya wa Ilala Jerry Slaa juu ya masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na muziki, siasa na afya pia

Meya Jerry Slaa akifafanua jambo katika mahojiano hayo

Baada ya mahojiano yaliyochukuwa takribani dakika 45 waliamua kupiga picha hiyo hapo
Kama unasumbuliwa na magonjwa sugu unaweza kufika Mandai Herbal Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838. Au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment