Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Friday, 13 March 2015

TIBA ASILIA ZA UGONJWA WA SARATANI
Kuna vyakula na matunda yenye uwezo wa kupambana au kuzuia ugonjwa wa saratani,lakini ufanisi wake hutegemea ukubwa wa tatizo hivyo mgonjwa anapaswa kupitia hospitali ili kupata ushauri na vipimo vinavyostahili kabla ya kuamua kutumia tiba hii.


Pia ni vyema ikafahamika kuwa tiba itakayoainishwa hapa hazipaswi kusimama kama tiba mbadala wa tiba za hospitalini, ingawa baadhi ya tafiti zimekuwa zikionesha kuwa na uwezo wa kupambana na tatizo hili kwa asilimia kubwa.

Yafuatayo ni matunda na vyakula vilivyo na uwezo wa kuzuia au kutibu saratani.

TUNDA LA STAFELI NA MTOPETOPE
Matumizi ya tunda hili mara kwa mara huweza kutibu na kuzuia saratani kwa kiasi kikubwa, hivyo tunda hili linapaswa litumike kila siku angalau mara mbilikwa kutwa
 
KABEJI
Andaa juisi yake kwa kuisaga kwenye mashine ya kutengenezea juisi kisha uinywe bila kuichija kwa kipimo cha vikombe vitatu kwa siku. 

Juisi hii huweza kuuzuia mwili usipate saratani za aina mbalimbali na pia inafaa kwa wagonjwa wa saratani walioanza matibabu.

TUNDA LA PARACHICHI
Tunda la parachichi linahitajika kutumika kwa wingi kutokana na uwezo wake wa kufyonza mafuta yanayoweza kusababisha saratani katika mwili.

Pia tunda hili lina kiasi kikubwa cha potasiamu ambayo ni nyingi zaidi ya kwenye ndizi na pia ni chanzo kikubwa cha beta carotene. Wanasayansi wanaamini kuwa tunda hili pia linauwezo wa kutibu Hepatitis ugonjwa ambao unaweza kusababisha saratani ya ini pamoja na vyanzo vingine vinavyopelekea kuharibika kwa ini.

MMEA  WA KAROTI
Mbali na hayo pia mmea wa karoti kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha 'beta- carotene' ambayo husaidia kupunguza uwezekano wa kupata aina nyingi za saratani zikiwemo saratani ya mapafu, saratani yam domo, koo, tumbo, utummbo, kibofu, tezi za matiti.

Chembechembe ya 'falcarinol' ambayo inapatikana katika karoti hupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa huo. Mara nyingi mboga hizi hupatikana katika masoko mbalimbali.

Endelea kufuatilia tovuti hii www.dkmandai.com, mara kwa mara nitaendelea kukujuza vyakula na matunda mengine ambayo huweza kukukinga na saratani au kumpatia ahueni mgonjwa wa saratani pia.

Mandai Herbal Clinic inaendelea kukukumbusha kwamba endapo unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu unaweza kufika kituoni kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata suluhisho la matatizo yako. Pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.  

No comments:

Post a Comment