Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 10 March 2015

TUMIA FURSA HII KUFAHAMU KUHUSU MAFUTA YA NAZI KATIKA TIBAMafuta ya nazi ni mafuta ambayo yamekuwa yakitumiwa sana na jamii za watu mbalimbali, huku kina mama wakionekana kupendelea zaidi kutumia mafuta haya kwa lengo la kuimarisha afya za nywele zao.


Mafuta ya nazi pia yamekuwa yakitumiwa sana kwa kuwapaka watoto wadogo hususani yale ambayo hayajachanganywa na kitu kingine chochote yaani yale yaliyo asilia.

Katika makala haya leo tutaangalia namna mafuta ya nazi yanavyoweza kutumika kama tiba ya matatizo mbalimbali kama ifuatavyo

Mafuta ya nazi yanauwezo wa kutibu fangasi wa miguuni, ambapo kinachohitajika ni kuchanganya mafuta ya mafuta ya nazi asilia pamoja na maji ya mchai chai, baada ya hapo utatumia mchanganyiko huo kupaka sehemu iliyoathirika.

Mafuta hayo pia huondoa madoa ya kwenye ngozi, hii mhusika atatakiwa kupaka mafuta hayo sehemu iliyoathirika mara mbili kwa siku kwa muda wa siku ishirini.

Pia mafuta ya nazi humsaidia mtu ambaye ameumwa na nyuki, ambapo kinachotakiwa kufanyika ni kupaka mafuta hayo sehemu ile aliyoumwa.

Kwa wale wenye tatizo la kuwa nachawa kichwani mafuta haya husaidia kuondosha tatizo hilo.

Mbali na hayo, mafuta ya nazi husaidia sana michubuko, ambapo utapaswa kuchovya mafuta kidogo na kupaka kwenye mchubuko unaweza kufanya hivyo mara mbili kwa siku asubuhi na jioni endelea hivyo hadi pale utakapoona tatizo limeisha.


Nitaendelea kukuletea umuhimu wa mafuta haya ya nazi, tafadhali endelea kuwa karibu na tovuti yetu hii.

Mandai Herbal Clinic inaendelea kukukumbusha kwamba endapo unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu unaweza kufika kituoni kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam na utapata suluhisho la matatizo yako. Pia unaweza kuwasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0752 163 838, 0682 368 443.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.  No comments:

Post a Comment